Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya ukarabati wa mabwene kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wanaofanya ukarabati huo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa mabweni nane yaliyofanyiwa ukarabati katika shule ya Sekondari ya wasichana
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa shule hiyo pamoja na maafisa wengine wakifanya ukaguzi wa majengo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Msalato Dodoma
Miongoni mwa mabweni yaliyokarabatiwa na serikali
Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana
ya Msalato Manispaa ya Dodoma wamemuahidi Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe.
Selemani Jafo kwamba watapambana ili katika matokeo ya kidato cha sita mwakani
shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora nchini.
Ahadi hiyo ilitolewa na wanafunzi hao katika ziara ya Naibu
Waziri Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu inayojengwa
na serikali ili kuirudisha shule hiyo katika hadhi yake.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule kongwe 88 zilizo katika mpango
wa ukarabatiwa na serikali ambapo ndani ya miaka 4 shule hizo zitakuwa ni shule
zenye ubora wa hali ya juu kwa kuboreshewa mazingira yake yakiwemo mabweni,
madarasa, vyoo, mabwalo, mifumo ya maji na umeme, pamoja na nyumba za
walimu.
Katika shule hiyo, serikali hadi sasa imeshakamilisha ukarabati
wa mabweni nane, mfumo wa umeme na maji.
Aidha Serikali imejipanga kuendelea na ukarabati wa madarasa na
ujenzi wa madarasa mengine manne mapya, ukarabati wa bwalo la chakula, majengo
ya utawala, na nyumba za walimu.
Kufuatia uboreshaji huo, Wanafunzi wameishukuru serikali na
wamemuahidi Naibu Waziri huyo kwamba watahakikisha wanajitahidi ili mwakani
shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita.
Akizungumza na wanafunzi hao, Naibu Waziri Jafo amewahakikishi
watanzania kwamba mpango wa serikali ni kuboresha shule za umma ili ziweze
kutoa elimu bora hapa nchini.
Mwaka jana, Naibu Waziri Jafo alitembelea shule hiyo na kuwataka
wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao
ili shule hiyo itoke kutoka shule ya 21 katika matokeo ya kidato cha sita mwaka
jana ili waingie 10 bora. Jambo ambalo katika matokeo ya mwaka huu shule hiyo
imeshika nafasi ya namba 14 kitaifa.
0 comments:
Post a Comment