SHIRIKA la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa
radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini.
Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.
Akizungumza wakati wakukabidhiana
vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na
radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
(kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio
jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema ni muhimu sana kwa
radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie
katika matata na kuchapisha au kutangaza stori baada ya kukamilika
kwake.
Alisema ipo haja kwa vyombo vya
habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba
hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia
maadili.
Meneja wa radio ya Jamii ya
Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na
kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano.
Meneja
wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la
shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya
vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege
Angulo.
Alishukuru UNESCO kwa kuwawezesha
kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada huo wataokoa shilingi
laki saba kwa mwezi kuazima transmita.
“Radio yetu inawafikia watu
500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia watu milioni 1
katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga Vijijini, Nyang’wale na
Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani Tabora ,” alisema meneja huyo .
Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka.
Ofisa
Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema
Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco
jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Ayubu Kalufya wa
radio ya jamii Uvinza alisema kwamba kituo chake kilikuwa kinakodisha
transmita kwash laki tano na kufanya kwa mwaka mzima kutumia sh milioni
6.
Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo.
Kwa mujibu wa Kalufya, transmita
hiyo mpya itawafikisha mbali zaidi katika pwani za Ziwa Tanganyika na
hivyo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.
Kalufya alisema wananchi wakisikia
mambo mbalimbali ya kuwaelimisha na wao wakapata nafasi ya kutoa maneno
yao haki za binadamu zitakuwa zimeheshimiwa sana nchini.
Mkurugenzi
wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya (kulia) akitoa neno la shukrani
kwa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya
radio hizo yaliyofanyika kwenye ofisi za shirika hilo jijini Dar es
Salaam.
Aliishukuru Unesco kwa kuendelea
kuwasaidia na kusema kama si kwa msaada wa UNESCO jamii zilizopo
pembezoni zisingepata nafasi ya kutoa madukuduku yao.
Radio nyingine zilizonufaika na msaada huo ni Pangani FM. Radio hiyo sasa inaweza kusikika Tanga nzima badala ya Pangani pekee.
Katika orodha ya redio zilizopatiwa vifaa ipo pia Mkoani FM ya kutoka Zanzibar.
Picha
juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Zulmira Rodrigues na Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya
Pangani FM, Rehema Kilapilo wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa
katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano
UNESCO.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa
Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo
wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini
Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya
mawasiliano Unesco Dar es Salaam.Picha
juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama,
Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo
katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano
UNESCO Dar es Salaam.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa
radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla
fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.Picha
juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya
kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla
fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa
Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya wakati wa hafla fupi
iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akigonga ‘cheers’ na wawakilishi wa redio jamii zilizopokea vifaa hivyo
kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Unesco
jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment