WAKATI Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, leo
wanaweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi hapa Tanga, Tanzania, maandalizi yote ya
uzinduzi wa mradi huo wa kihistoria yamekamilika, humu mji ukifurika na
kupeleka neema kwa wafanyabiashara wa nyumba za wageni, vyombo vya
usafi ri na kadhalika.
HabariLeo jana lilitembelea Chongoleani na kukuta wahusika
wakikamilisha ujenzi wa jukwaa, upangaji viti na uwekaji wa mahema. Juzi
katika eneo hilo hilo, gazeti hili pia ilishuhudia wazee wa eneo mitaa
ya Putini na Chongoleani wakiomba dua ili shughuli ya leo na
zitakazoendelea kufanyika katika eneo hilo zipate baraka za Mwenyezi
Mungu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na Meya wa Mji wa Tanga,
Seleboss Mustafa, wamewataka wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi
kushuhudia uwekaji huo wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba hilo
linalotazamiwa kuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa
Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Saturday, August 5, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ...
-
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dkt. Titus Kamani, akizungumza na viongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Walimu ...
-
HOTUBA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ISIMANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWAKA 2015 UTANGULIZI UTA...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment