Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KAMANDA wa polisi mkoani
Pwani,(ACP),Jonathan Shanna ametoa wiki moja kwa wazazi na walezi
wanaowanyima watoto wao haki ya elimu kwa kuwaingiza katika ndoa za
utotoni na wengine kutumikishwa kazi za kijamii kuwapeleka shule kabla
hawajachukuliwa hatua.
Amesema kutokana mambo hayo atakuwa mkali na wanatarajia kuanza operesheni ya kuwafichua wazazi wanaokatisha masomo watoto .
Aidha amesema jeshi la polisi
mkoani hapo limekamata silaha tatu katika wilaya ya kipolisi
Mlandizi,Kibaha na Bagamoyo, ikiwemo shortgun isiyokuwa na namba ikiwa
imekatwa mtutu,RIFLE MARK na shortgun yenye namba 68687.
Akizungumza wakati akikagua
gwaride maalum kwa askari mjini Kibaha,kamanda Shanna
alieleza,haikubaliki/haiwezekani kuwa na mkoa wenye lundo la watoto
wasio na elimu.
Alisema watashirikiana na
watendaji wa vitongoji,kata na maafisa elimu ili kuhakikisha elimu kwa
watoto ipewa kipaumbele kuendana na kasi ya rais dk.John Magufuli.
Alisema watakwenda nyumba kwa
nyumba,shamba kwa shamba kuwafichua watoto waliofichwa na watawachukulia
hatua wazazi ambao watakiuka agizo hilo.
“Nitakuwa mkali zaidi ya
pilipili,”watoto wote walioachishwa shule warudi shuleni mara moja,na
wazazi walioshiriki kuozesha watoto watachukuliwa hatua a kisheria ambao
haijawahi kutokea duniani.”
“Kuna tabia ya watu kuhamia
mashambani tutawafuata mashambani,tutakwenda hadi huko,askari wangu wana
molari,wapo vizuri hadi Pwani itakapokuwa shwari kwa mikakati
yake”alisema .
Hata hivyo kamanda Shanna alisema pia wanapambana na madawa ya kulevya na kufanikiwa kukamata bangi kg moja na heroin gram 1.20.
Alisema pia huko wilaya ya
kipolisi Chalinze ilifanyika operesheni na kufanikiwa kukamata mitambo
miwili ya kutengeneza pombe ya moshi .
Kamanda huyo,alieleza,wanaendelea
na misako na doria mbalimbali katika maeneo ya mkoa wa Pwani,kuhakikisha
wanatokomeza uhalifu kwa kiasi kikubwa .
Kamanda Shanna ,alitoa rai kwa
wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwafichua
wahalifu waliopo kwenye maeneo yao ili waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Alisema kwa kufuata mikakati
waliojiwekea ikiwa ni sanjali na operesheni ya kuwafichua watoto
waliokatishwa masomo yao na kupunguza uhalifu anaamini watafanikiwa
kutokomeza changamoto hizo na uhalifu mkoani hapo .
Baadhi
ya wananchi wilayani Kibaha,akiwemo Amina Shaha na Jumanne Anas
walisema kufanyika kwa operesheni hiyo ya kuhakikisha watoto
waliokatishwa masomo wanapelekwa shule ni jambo jema .
Anas alisema jukumu la wazazi ni kuwainua watoto wao katika suala zima la kuwapa elimu .
Amina
alieleza,wapo baadhi ya wazazi ambao wanawatumikisha watoto wao kuuza
biashara za familia kama karanga,mbogamboga na wengine kuwaozesha wakiwa
wadogo.
Alisema tabia hiyo ikomeshwe ili iwe fundisho kwa wazazi wenye tabia hizo.
0 comments:
Post a Comment