METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 30, 2017

TIGO YAMUUNGA MKONO MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA KWA KUTOA MADAWATI

Kampuni ya Huduma za Simu nchini ya Tigo leo imeamua kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kumkabidhi madawati Mia Moja kwa lengo la kupunguza changamoto za utoaji wa Elimu ili kuimarisha sekta hiyo Jimboni humo  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yao kwake

Akizungumza wakati wa upokeaji wa madawati hayo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuishukuru Kampuni ya Tigo kwa namna inavyojitoa katika kusaidia huduma mbalimbali za kijamii  amesema kuwa Tigo imekuwa kampuni inayowajibika kwa kutekeleza ahadi zake inazozitoa

‘… Kwakweli tunawashukuru wenzetu wa Tigo wamekuwa wakitekeleza kile inachokiahidi na tumekuwa na mahusiano nao mazuri na ninaimani tutaendelea kusaidiana, Tigo ni watu wasikivu wakiahidi wanatoa na wakisema hawana basi inakuwa ni kweli hawana …’ Alisema

Aidha Kampuni hiyo ya Tigo imepanga kusambaza Simu za Mezani kwa Shule za Jimbo la Ilemela lengo likiwa ni kurahisisha Mawasiliano ndani ya Jimbo hilo

Kwa upande wake Meneja wa Tigo  Mkoa wa Mwanza Ndugu Kassim Aziz  amesema kuwa huu ni muendelezo wa Kampuni yake katika kuunga mkono Serikali na Mbunge wa Jimbo la Ilemela kuhakikisha yanakuwepo mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia sanjari na kupunguza changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu

Makabidhiano hayo yalihusisha pia Viongozi wa Manispaa ya Ilemela akiwemo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe Renatus Mulunga na Mkurugenzi wake John Wanga wakiwa na Kamati ya Fedha ya Manispaa hiyo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
30.08.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com