Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mmoja wa viongozi wa Shirika
linaloshughulikia wakimbizi NHCR katika Kambi ya Nduta Kibondo mkoani
Kigoma.
Baadhi ya wakimbizi wakijisajili kurejea nchini kwao Burundi.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mwigulu Nchemba akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika
linaloshughulikia wakimbizi kambi ya Nduta Kibondo mkoani Kigoma
…………………………………………………………………………………
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mwigulu Nchemba ametoa siku saba kwa shirika la wakimbizi Duniani (
Tanzania) kukamilisha taratibu za kuwarudisha warundi waliomba kwa
ridhaa yao kurudi nchinj kwao Burundi.
Waziri Mwigulu amefikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa ya
watu 8,743 ambao wamejisajili kwa hiari yao kurudi burundi wakiwa
katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani kibondo mkoa kigoma, lakini
wanakwamishwa na shirika la UNHCR ambalo wanasema wanataka kukaa vikao
ndio waweze kiwarudisha.
Waziri Mwigulu amesema baada ya siku saba endapo UNHCR
watashindwa kuwapeleka kundi la kwanza kwao basi yeye ataongea na waziri
wa ulinzi kuomba kwa Amri jeshi mkuu Rais Magufuli magari ya
kuwarudisha wakimbizi hao makwao.
Kwa upande wa mkuu wa makazi ya Nduta Peter Bulugu amesema
kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na kati ya hiyo
watu 8,743 wameomba kurudishwa makwao na kuchelewa kurudishwa kuna
pelekea sasa hali ya usalama kuwa si nzuri kwani kunawepo na vitendo vya
vurugu za mara kwa mala kutoka kwa wakimbizi hao wanaotaka kuondoka.
Mkuu wa makazi amesema kupunguzwa kwa chakula kumechangia
kuongezeka vitendo vya wizi ndani na nje ya kambi (wizi wa mifugo na
mazao mashambani wizi wa taa za mitaani kambini (48 kati ya 217
zimeibbiwa) utekaji na ubakaji barabarani umeongezeka sasa.
Moja ya wakimbizi ambaye alikutwa anajiandikisha kurudi kwao
amsema ameamua kujiandikisha baada ya kuambiwa kuna usalama kwao lakini
pia changamoto wanazo kutana nazo za kupunguzwa kwa chakula walichokuwa
wanapata mwanzo mpaka sasa kufikia kula mlo moja kwa siku ameona bora
arudi kwenda kuwai muda kilimo
0 comments:
Post a Comment