Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Singida ACP Debora Magiligimba akionyesha bunduki aina ya rifle iliyokuwa
ikimilikiwa na mtuhumiwa wa ujambazi Hamisi Athumani (32) mkazi wa
Shiponga-Hanang mkoa wa Manyara anayedaiwa kuitumia kwenye matukio ya ujambazi.
Na Nathaniel Limu
Mkazi
wa kijiji cha Shiponga – Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi
Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi
wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea
Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya
Ngimu wilaya ya Singida.
Amefafanua
kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu
kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na
risasi zake tano.
Amesema
bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa
kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na
kufichwa chini ya jiwe.
ACP
Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa
kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa
tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.
“Kesho
yake mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi wa
kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka askari
kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio hayo ya
ujambazi”, amesema ACP Magiligimba.
Kamanda
huyo amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa na mtuhumiwa,
walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali alipokuwa ameficha bunduki
hiyo aina ya rifle.
“Mara
tu baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea
kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari kwa
kukimbia” amesema na kuongeza;
“Askari
mmoja alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii. Ndipo
alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.
Amesema
jereha hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi, na hivyo
kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.
“Jeshi
la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote kutoa
taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili hatua ziweze
kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu”, amesema kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment