METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 29, 2017

MTOTO ALIYEZALIWA BILA MACHO AFARIKI DUNIA

Mtoto wa kike aliyezaliwa na ulemavu sehemu ya uso amefariki dunia baada ya mama yake kugoma kumnyonyesha maziwa.

Mtoto huyo alizaliwa jumapili Agost 27 bila macho na pua ikiwa juu ya paji la uso. Kwa mujibu wa familia, mama wa mtoto huyo Mariam Mwakombo (22) aligoma kumnyonyesha kwani alikuwa akiogopa.

“Mtoto nilijifungua usiku na alikuwa akilia sana ila niliogopa kumshika kwani alikuwa na maajabu” aliliambia gazeti la Kenya Nation.

Mwakombo alihudhuria mara mbili kliniki ya kijiji cha Kilifi kwa muda wote mpaka kujifungua na wanakijiji walipanga kumtupa mtoto huyo lakini baada ya kufariki dunia walimzika nje ya nyumba ya familia.

Source: Kenya Nation Newspaper.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com