Baadhi ya madiwani wa Baraza
hilo,wakifuatilia taarifa ya mwanasheria wa halmashauri juu ya madai
ambayo wanahudai mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)
Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo,Leornad
Kiganga Bugomola,akielezea msimamo wa baraza la madiwani wa Halmashauri
hiyo juu ya madai ya mgodi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akijibu baadhi ya maswali.
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini.Constatine Kanyasu akichangia ajenda ya swala la malipo ya mgodi kwa halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa mgodi wa GGM Kwenye baraza Hilo Bw Joseph Mangilima akitoa ufafanuzi juu ya madai ambayo yanadaiwa na Halmashauri.
Halmashauri ya mji wa Geita imeitaka
kampuni ya madini ya dhahabu ya Geita (GGM) kulipa kiasi cha dola za
kimarekani zaidi ya milioni 11.045 ambazo ni madai ukwepaji wa kodi ya
huduma kwa kipindi cha mwaka 2004 hadi 2013 nakuipa muda wa mwezi mmoja
endapo itashindwa itaupeleka Mgodi Mahakamani.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Eng.
Modest Apolinary,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine
Kanyasu,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine
Morandi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola.
Mgodi wa GGM ulianza uzalishaji mwaka 2000 na kuingia makubaliano na
Wizara ya nishati na madini ya kulipa dola 200,000 kwa halmashauri kila
mwaka lakini inadaiwa haikulipa hadi mwaka 2004 kwa madai kuwa
halmashauri haina sheria inayoelekeza walipwe kiasi hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amesema
kuwa wametoa siku 30 fedha zilipwe na endapo hawatalipwa basi
wataupeleka mgodi Mahakamani kwakuwa sheria zipo wazi inayowataka kulipa
asilimia 0.03
Awali akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwanasheria wa
Halmashauri ya mji Queen Luvanda amesema Madai hayo yanatokana na kodi
ya huduma ambayo kampuni ilipaswa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka 2004 Halmashauri ilitunga Sheria ndogo ya kodi ya huduma ya
asilimia 0.03 ya mauzo ya mwaka na kuanzia sheria itungwe mgodi
hawakulipa asilimia 0.03 bali walilipa dola laki mbili kuanzia mwaka
2004 hadi 2013 kinyume na maelekezo ya sheria inavyosema.
Maneja Kitengo cha Mahusiano katika Mgodi wa GGM Joseph Mangilima
amesema sheria ya kodi ya huduma ilitungwa mwaka 2004 na ikaanza kufanya
kazi mwaka 2005 na Kampuni ilikua ikilipa dola 200,000 kila mwaka kwa
mujibu wa sheria
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
0 comments:
Post a Comment