Waziri
wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amesema kuwa hakuna
tishio lolote la hivi karibuni kutoka Korea Kaskazini , licha ya
Pyongyang kusema kuwa inapanga kushambulia eneo la Guam nchini Marekani.
Kuhusu Guam bwana Tillerson pia alimtetea rais Donald Trump ambaye ameitishia Korea Kaskzini kwamba ataikabili kivita.
Alisema kuwa rais Trump alitaka kutuma ujumbe kwa Korea Kaskazini.
Lakini rais huyo amejigamba katika mtandao wa Twitter kuhusu uwezo mkubwa wa zana za kinyuklia za Marekani.
Katika
ujumbe wa mtandao wa Twitter uliochapishwa mwendo wa Alfajiri, rais
Trump alisema kuwa silaha za kinyuklia za Marekani zimeimarika zaidi ya
ilivyokuwa lakini akasema kuwa anatumai hatalazimishwa kuutumia uwezo
huo.
Ujumbe
huo wa Twitter unafuatia kuzuka mwa majibizano kati ya pande hizo mbili
huku kisiwa hicho cha Guam ambacho ndio makao ya ndege za kivita za
Marekani na watu 163,000 kikizungumziwa.
"Huku
idara yetu ya maswala ya kigeni ikifanya kila juhudi ya kutatua swala
hilo, kwa njia ya kidiplomasia ni lazima ifahamike kwamba jeshi la
Marekani limeimarika na lina ulinzi mkali duniani''.
''Vitendo vya Korea Kaskazini vitashindwa na majeshi yetu itapoteza silaha na migogoro inayolenga kuanza'', aliongezea.
0 comments:
Post a Comment