Mtindo wa karate mkongwe
duniani, Okinawa Goju Ryu wa chama cha Jundokan Tanzania chini ya
mwakilishi wake Sensei Rumadha Fundi mwenye Dan 4,“Yondan” pia mwenye
uzoefu wa zaidi ya miaka 38 ya mafunzo ya sanaa ya Karate mtindo wa Goju
Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan kama vile
Master Mario Higaonna(IOGKF), Master Masataka Muramatsu( Goju Ryu
Kyokai), Teruo Chinen( Jundokan International), na hatimae Kancho
Yoshihiro Miyazato, mwenyekiti wa (Jundokan So Honbu, Naha,
Okinawa)Master Tetsunosuke Yasuda, Master Tsuneo Kinjo na Master Tetsu
Gima.
Tunatarajia kufanya
mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “
Kaizen dojo” Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo.
Hii ni moja ya jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia
ufundishaji wa mbinu za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama
“Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote
itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus” ya
Jundokan, Okinawa.
Lengo pia ni
kuzungumzia yale yote yaliojiri katika semina kuu ya Jundokan bara la
Ulaya chini ya master wake toka jijini Naha, Okinawa mwezi wa Julai
2017. Ufundishaji sahihi wa mfumo huu ni moja ya malengo kuhakikisha tu
kwamba wana Jundokan duniani mkote wapo kwenye msimamo mmoja katika
uchambuzi na ufanyaji wao wa Kata na matumizi yake.
Pia wakati huohuo,
kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda mieusi wa Jundokan
Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha wanafunzi wake
kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji Kata kama jinsi
ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo huo unaofuata
nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa mtindo wa
Okinawa Goju Ryu.
Hivyo, hii ni moja
ya fursa kubwa kwa wana Jundokan kuweza kushiriki semina hii chini ya
mwakilishi wa Jundokan Tanzania, ama kamaijulikanavyo “Tanzania
Shibu-Cho”, sensei Rumadha Fundi. Sensei Rumadha, amesisitiza kwa niaba
ya chama hicho kwamba Kila mwanafunzi wa mkanda mweusi, hana budi
kuhudhuria semina za walimu angalau mara moja kila miaka miwili na
kupata usahihisho muhimu kimafunzo. Hilo ndio lengo kuu hata kipindi
kile kwa mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania, marehemu Sensei NC
Bomani kufanya ziara za mara kwa mara kwenda huko Naha, Okinawa kupata
marekebisho toka kwa magwiji wa Karate duniani na chimbuko lake.
Pia vilevile,
Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tokea
kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018 mjini Naha,
Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master
Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia alikuwa ndio
mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au
mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha, hamna mabadiliko yeyote
kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa akifundisha mwanzilishi
wake Chojun Miyagi sensei.
0 comments:
Post a Comment