METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 10, 2017

DKT TIZEBA: TUMEDHAMIRIA KUBORESHA SEKTA YA UVUVI ILI KUONGEZA UZALISHAJI NA TIJA


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi  tarehe 8 Agosti 2017.

Na Mathias Canal, Lindi

Serikali imetangaza dhamira ya kuhakikisha kuwa inaboresha zaidi Sekta ya Uvuvi ili kuongeza uzalishaji na tija, ikiwa ni pamoja na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba  amesema hayo wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, nane nane kitaifa, katika viwanja vya Ngongo katika manispaa ya lindi jana tarehe 8/8/2017.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo serikali itahamasisha watu wengi kufuga samaki katika mabwawa na vizimba ili waweze kuzalisha samaki wengi zaidi sambamba na kuboresha zaidi uvuvi wenye tija na ambao ni endelevu. 

Dkt Tizeba amemshukuru  Mhe. Makamu wa Rais kwa hatua zizochukuliwa  na Ofisi yake za kulinda mazingira ya nchi, ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa cheti cha kukidhi matakwa ya utunzaji mazingira.

Alisema ipo Mipango mbalimbali iliyowekwa na wizara, hivyo itatekelezwa kwa ufanisi zaidi kwa kuhimiza ushiriki wa Sekta Binafsi, kuwekeza zaidi katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kuzingatia mnyororo wa thamani ili kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo au kabla ya mwaka 2025. 

Alisema jambo hilo linaendelea vyema kwa kuhuisha kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2017 isemayo; Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati

Dkt Tizeba aliongeza kuwa Kupitia Kaulimbiu hiyo wizara yake inahimiza, matumizi ya nyenzo sahihi kama matrekta, na mashine nyingine za uzalishaji na usindikaji, kuongeza uwekezaji katika viwanda vodogo,  vya kati na vikubwa,  sambamba na kuweka mazingira bora yanayovutia Sekta Binafsi kuwekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia mnyororo wa thamani.

Aidha, alisema kuwa katika Maadhimisho hayo, Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika na Wadau wengine walipata nafasi ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na hatimaye Sekta ya kilimo iweze kuongeza uzalishaji na tija zaidi. 
Aliongeza kuwa uzalishaji, wizara itajihakikishia ziada kubwa ya chakula na malighafi za kutosha katika viwanda vilivyopo na vinavyotarajia kuanzishwa. Kama ambavyo, inafahamika kuwa upatikanaji wa masoko ya uhakika, utachochea zaidi uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, uhakika wa bei kwa mazao na bidhaa zinazozalishwa na Mkulima, Mfugaji na Mvuvi atakayewekeza zaidi katika uzalishaji.

MWISHO
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com