METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 9, 2017

Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kuwahoji waliokuwa viongozi wa TASO Kanda ya Mashariki

Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwakamata mara moja waliokuwa viongozi wa chama cha wakulima Tanzania TASO kanda ya mashariki kutokana na ubadhirifu wa fedha  walioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. 
Dk Kingwangala alitoa agizo hili mara baada ya kupokea taarifa za kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mh. Dk. Steven Kebwe  juu ya walioukuwa viongozi wa Taso kanda ya Mashariki kushirikiana kuuza baada ya maeneo kwa wananchi ndani ya uwanja wa maonyesho ya mwalimu Juliaus Nyerere nanenane ulipo mkoani Morogoro. 
Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho cha Nane nane akimwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Salum, ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka viongozi hao  huku akieleza kuwa kutokana na usajili wamashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa ndani ya wizara yake ni, vyema viongozi hao wakatafutwa na kukamatwa ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili. 
“Kwa mamlaka, tunawaagiza Mkuu wa TAKUKURU kuhakikisha wanawakamata viongozi wa TASO haraka ilikuweza kurudisha mali zote ikiwemo walizowauzia wananchi viwanja ndani ya maeneo haya. Taasisi ama NGO’s zikifilisiwa mali zote ni za Serikali na zinakuwa chini ya uangalizi wa Serikali hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wale waote waliohusika” alieleza Dk. Kigwangalla katika tukio hilo la kufunga kilele cha maadhimisho ya Nane nane, Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar e s Salaam,  katika Banda la Mwalimu Julius Nyerere. 
Dk. Kigwangalla apia ameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Vyeti, hundi za fedha pamoja na vikombe vya ushindi kwa taasisi na mashirika na wadau walioshiriki maonyesho hayo. 
Hata hivyo Dk. Kigwangalla ameongeza siku mbili zaidi kuendelea kwa maonyesho hayo ambayo yaendelea leo na kesho  Alhamisi Agosti 10,2017. 
Awali amepata Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya viwanja hivyo  huku akijionea mazao ya kilimo na ufugaji wa kila aina pamoja na bidhaa zitokanazo na kilimo za wadau wa ndani.
Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akipokelewa wakati akiwasili viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia namna mashine ya kukoboa mahindi ya kisasa inavyofanya kazi ambayo itakuwa msaada kwa wakulima  hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiwasabahi baadhi ya watoto waliofika kwenye  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Baadhi ya viongozi wakiangalia bidhaa za ngozi kutoka kwa  Mjasiriiamali  kutoka Tanga kwenye maonyesho hayo  
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia mazao ya shambani kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia mazao ya shambani kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Moja ya bwawa la Samaki la kisasa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiangalia moja ya mabwawa ya samaki ya kisasa kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akipata maelezo namna ya upandaji wa mazaoo ya miwa maalum kwa sukari  kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo  kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Baadhi tya viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa kilimo wakifuatilia tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akikabidhi vyeti kwa washiriki kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akikabidhi kombe la ushindi kwa washiriki kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akijadiliana na wadau wa Kilimo hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com