METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 19, 2017

DC MUFINDI: NI AIBU MIAKA 55 YA UHURU BADO KUNAWATANZANIA NANAJISAIDIA PORINI

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akikata utepe, kuzindua huduma ya Maji uliokarabatiwa na Shirika la PDF.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi akipokea Risala ya Shirika la PDF
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akiwahutubia wananchi wa wakati wa uzinduzi wa mradi kata ya Mbalamaziwa

NA OFISA HABARI MUFINDI    
                                                                                          
Serikali Wilayani Mufindi, imesema itaanza kuchukua hatua kali za kisheria zilizopo kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wasiozingatia sheria za afya ya mazingira, hususani suala la kuwa na vyoo, ambapo takwimu zinaonesha kati ya kaya 59,152 za Halmashauri hiyo, zaidi ya kaya 7,00 hazina vyoo huku kaya zaidi ya 3,000 bado zinatumia vyoo vya asili.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh Jamhuri William, katika kata ya Mbalamaziwa alipokuwa akizindua mradi wa Maji, Afya, Lishe, usafi wa Mazingira sanjari na usafi wa Mtoto chini ya miaka 05 ukitekelezwa kwa pamoja kati ya Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la (peoples Development Forum) PDF chini ya ufadhili wa UNICEF.

Mh. Jamhuri amesema ni aibu kwa muda wa miaka 55 ya uhuru bado kuna Watanzania wanajisaidia porini au kwenye vyoo visivyo na sifa na kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira pamoja na magonjwa ya mlipuko na kufafanua kuwa suala la kuwa na nyumba bora linalozingatiwa na wakazi wa Halmashauri hiyo, ni lazima liende sambamba na ujenzi wa choo chenye ubora huku akiahidi kuchukua hatua za kinidhamu kwa watendaji wa Vijiji watakao zembea kusimamia suala hilo.

Katika hatua nyingine Mh. Jamhuri William, amewataka wakazi wa Halmashauri hiyo, kutumia vema uwepo wa aina mbalimbali za vyakula  Wilayani humo, kuondokana na suala la lishe duni licha ya Mkoa wa Iringa kuwa miongoni mwa mikoa 05 ya nyanda za juu inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula, huku akitilia mkazo kuachana na tabia ya kula unga wa Sembe badala ya dona yenye viinilishe hitajika.

BDF Kwa kushirikiana na Halamashauri ya Wilaya ya Mufindi chini ya ufadhli wa UNICEF, itatekeleza miradi hiyo katika kata nne za Mbalamaziwa, Ikweha, Sadani na Mtambula, ambapo itachimba visima, kukarabati miradi ya Maji, Ujenzi wa vyoo kwenye tasisi za umma pamoja na Usafi na lishe bora kwa Mtoto chini ya miaka 05
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com