Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii wa Nyimbo
za Injili (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wasanii hao kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Chama cha
Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akifafanua jambo wakati
wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto
zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili
Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba akiwasilisha changamoto
zinazokabili muziki wa injili hapa nchini wakati wa mkutano na wasanii
wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya
kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili
Bi. Christina Shusho akichangia hoja wakati wa mkutano na wasanii wa
nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua
changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa nyimbo za Injili
wakitumbuiza wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha
ya pamoja na viongozi kutoka serikalini pamoja na viongozi wa chama cha
Muziki wa Injili Tanzania baada ya mkutano na wasanii hao kujadili
changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini
Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za
Injili leo Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili
tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua
changamoto hizo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mkutano na
wanamuziki wa nyimbo za Injili Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali ina
wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa
injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu
mmoja mmoja na taifa.
“Muziki ni tasnia ambayo imewabeba
vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda na
kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili
inaheshimiwa na kulindwa” Amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare amewataka
Wasanii wa Muziki wa Injili kutoshawishiwa kutoa malipo yoyote katika
vyombo vya habari ili nyimbo zao ziweze kuchezwa kwenye vyombo hivyo
bali vyombo vya habari ndio vinapaswa viwalipa wasanii wakati
wanapotumia nyimbo zoa.
Aidha Bibi. Doreen amewaomba
waimbaji hao wa nyimbo za injili kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu,
Cosota na Basata ili waweze kupata ushauri wa namna ya kuandika mikataba
bora na inayofaa wakati wa kutengeneza na kuandaa albamu za nyimbo za
injili.
Naye Rais wa Chama cha Muziki wa
Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba amewataka Viongozi wa nyimbo
za Injili Tanzania kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bega kwa bega na
serikali na kwa bidii katika kukuza, kuendeleza, na kulinda maslahi ya
wanamuziki wa Injili.
Aidha Bw. Novemba ameiomba
serikali kuhusisha wanamuziki wa nyimbo za injili katika matukio
mbalimbali ya serikali na ya nchi kwani wasanii wa nyimbo za injili
wamekua wakiimba nyimbo zinazojenga taifa na kuendeleza amani, upendo na
ushirikiano wa nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment