Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo ya
bidhaa za mafuta aina ya petroli kwa Agosti , ambazo zimeendelea kushuka
kwa miezi minne mfululizo kuanzia Aprili.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura,
Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo zimeshukwa kwa Sh36 na
Sh44 kwa lita ya petrol na dizeli mtawalio.
Taarifa
hiyo inasema kwamba tofauti ni katika mafuta ya taa ambapo bei yake
imeongezeka kwa Sh24 kwa lita, hali iliyosababishwa na kuongezeka kwa
gharama ya usafirishaji wa bidha katika mfumo wa Uagizwaji wa Mafuta kwa
Pamoja (BPS).
Wastani wa matumizi ya mafuta kwa siku ni lita milioni tano, milioni tatu na 100,000 kwa dizeli, petrol na mafuta ya taa, sawia.
Kutokana
na bei hizo mpya, kuanzia leo lita moja ya petrol katika jiji la Dar
es Salaam itauzwa kwa Sh1,978 kutoka ilivyokua mwezi uliopita ya
Sh2,014, wakati lita ya dizeli sasa itauzwa Sh1,830 kutoka Sh1,874 na
mafuta ya taa yatapanda mpaka Sh1,830 kutoka Sh1,806 kwa lita kwa mwezi
uliopita.
Mhandisi
Samweli amesema kwa Mkoa wa Tanga, hakutakuwa na mabadiliko kwa petroli
na dizeli kwa sababu hakuna mzigo uliopokelewa kupitia bandari ya Tanga
kwa mwezi wa saba 2017. Hii itafanya bei za bidhaa hizo kwa mkoa huo
kubaki kama zilivyokua kwa mwezi wa saba 2017.
“Pia,
kwa kuwa hakuna bidhaa mpya ya mafuta ya taa iliyoingizwa kupitia
bandari ya Tanga, wafanyabiashara wanashauriwa kuchukua bidhaa hiyo
kutoka mkoa wa Dar es Salaam na pia, bei ya mafuta ya taa kwa mkoa wa
Tanga zitategemea na gharama za mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia
bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam
hadi Tanga”, amesema.
Kwa
upande wa waendesha magari ambao wangependa kupata bei za mafuta,
wanaweza kupata bei kikomo kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga
*152*00 na kisha kufuata maelekezo.
Taarifa
ya Ewura inasema puia kuwa kampuni za kuuza mafuta ziko huru kuuza
bidhaa zao katika bei ya ushindani yenye faida, isipokuwa wazingatie
kuwa bei hizo hazizidi bei elekezi.
==> Hapo chini ni Taarifa nzima ya EWURA
0 comments:
Post a Comment