METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 25, 2017

SHAKA:CCM HAIOKOTI VIONGOZI BARABARANI KAMA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) pamoja na Wanachama ,Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake wakiwa na shamra shamra  alipowasili katika kikao cha ndani pa
 Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM  Wilaya ya Nyamagana bi:Odilia Batimayo akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL.
  Baadhi ya mabango yakiwa na jumbe mbalimbali kwa ndg:Kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa ccm Ndg:Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg:Hussein Kim akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
Naibu Mstaiki Meya wa jiji la mwanza Mhe: Biku kotecha akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
 Mbunge wa jimbo la nyamagana Mhe:Stanslaus mabula  akisalimia na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya mbunge jimbo la nyamagana kwa vijana katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
ndg:Rooben Sixbert Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mwanza  akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) kuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zakekatika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL
   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  akuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

Na Mathias Canal, Nyamagana-Mwanza

Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake zote hakiokoti wanachama barabani, uchochoroni, ama mtaani kama ilivyo katika vyama vingine ambavyo sio CCM.

Umoja huo umesema kuwa kuokota Viongozi barabarani ni kuzalilisha Chama na Jumuiya zake na kupoteza Misingi ya uwajibikaji na utendaji ya kupata viongozi walioandaliwa kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Mpaka Taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 25, 2017 katika Ukumbi wa BELMOUNT FIRMOUNT HOTEL uliopo Manispaa ya Nyamagana Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na  wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM).

Shaka alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hufanya maandalizi ya uchaguzi Mkuu pindi tu unapomalizika uchaguzi kwa kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza Kusimamia na kufatilia utekelezaji wa ilani ya ushindi ya CCM.

Alisema kuwa anavionea huruma vyama vya upinzani kwani havitaweza kuwa na mgombea Mwenye uwezo wa kushindana na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwani kazi kubwa anayoifanya nchini katika kipindi cha utendaji wake kinaungwa mkono na Wananchi wote wakiwemo wale wa Chama vya upinzani na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

"Vijana wenzangu napenda mtambue kuwa siku zote Kizuri Chajiuza na kibaya chajitembeza, Hivyo Rais Magufuli ni KIZURI ambacho kinajiuza chenyewe bila hata kutembezwa na mtu yeyote" Alisema Shaka

Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kushinda kwa haki, Amani na Demokrasia pasina vurugu, Ghubu, na visilani kama inavyofanywa na vyama vingine visivyo CCM.

"Nataka niwakumbushe tu ndugu zangu wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa nchi yetu ya Tanzania haijawahi kuwa na vyama vya upinzani Bali imewahi kuwa na vyama vya vurugu na kejeli dhidi ya Serikali yao" 

"Ninazo taarifa kuwa kuna Kata moja wamepitishwa wahenga kwenye uchaguzi wa Vijana sasa natoa maelekezo kwa Katibu wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza kusimamia na kuwatoa haraka kwani wakiwaacha mpaka wakaingia kwenye uchaguzi watakuwa wamekiuka taratibu na Kanuni za Uchaguzi" Alisisitiza Shaka

Katika Ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo ameshiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini na kuahidi kumalizia katika upauaji jambo ambalo limemfanya pia Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kuchangia Bando tatu za bati ili kumuunga mkono Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka.

Aidha, Shaka ameshiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Mawe yenye urefu wa Kilomita moja kwani itatoa urahisi wa Huduma za kijamii hususani kwa Wakati wa Kaya ya Mahina na Kata ya Pamba.

Shaka amesisitiza mipaka ya kazi na kuwepo heshima kwa kuchagua viongozi wenye sifa za kuchaguliwa huku akiwakumbusha Vijana Kujiunga katika vikundi Mbalimbali ambavyo watavisajili na hatimaye kuandika barua ya kuomba mikopo ambayo inatolewa na Serikali kwa riba nafuu ya shilingi 50,000 kwa kila wanapokopa Milioni Moja.


MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com