WAZIRI wa Nchi Ofisi
ya Rais TAMISEMI George Simbachawene ameahidi kumfikishia Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli ombi la kuitangaza Manispaa ya Dodoma
kuwa Jiji kwani inakidhi vigizo na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kupewa hadhi
hiyo.
Alitoa ahadi hiyo
jana wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Dodoma katika Ukumbi wa
Shule ya Sekondari ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika
Manispaa hiyo, iliyojumuisha pia ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo.
Aidha, amewataka
watumishi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao (CDA) kumshukuru Rais kwa
uamuzi wa kuivunja Mamlaka hiyo kwa sababu hatua hiyo imeondoa mkanganyiko
uliokuwepo katika kuhudumia wananchi hususani katika sekta ya ardhi na mipango
miji ambako Manispaa ya Dodoma pia ilikuwa na jukumu hilo.
0 comments:
Post a Comment