METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 6, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AZINDUA MRADI WA UFATUAJI MATOFALI KWA VIJANA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amezindua mradi wa ufatuaji matofali yatakayosaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa sambamba na kuwainua kiuchumi vijana wa Jimbo la Ilemela unaotekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi ya The Angeline Foundation kwa ufadhili wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC

Akizungumza  na Vijana walioshiriki mafunzo ya awali ya utekelezaji wa mradi huo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kushukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa namna linavyounga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli amewataka Vijana wa Jimbo la Ilemela kujituma kwa kuzitumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazojitokeza  huku akiwaasa juu ya kuwa waaminifu na kuacha kuchagua kazi

‘… Kwa nafasi ya pekee nilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa namna mnavyounga mkono jitihada za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli lakini nitumie hadhara hii kuwaomba vijana wa Ilemela kujituma kuhakikisha Jimbo letu linapiga hatua kimaendeleo kwa kufanya kazi na si kuchagua kazi lakini pia muwe waaminifu kwa kila mnachokifanya tukifanya hivyo nchi yetu itapiga hatua kwa haraka sana …’ Alisema

Nae Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Mkoa wa Mwanza  Injinia Benedict Kilimba         amemuhakikishia Mbunge huyo kuwa Shirika lake litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha inawaletea waTanzania maendeleo kwa kufanya kila kinachowezekana kilicho ndani ya uwezo wao kuhakikisha miradi inayotekelezwa na Serikali inakamilika kwa wakati na kwa gharama nafuu

Kwa upande wa vijana walioshiriki zoezi hilo wamemshukuru Mbunge wao Dkt Angeline Mabula na kumhakikishia kuwa wataendelea kuthamini jitihada anazozifanya za kuhakikisha anasaidia Vijana kuweza kujikwamua kiuchumi hasa kwa kujitegemea na kuacha kufikiria kuajiriwa peke yake kama ndo njia ya kujikwamua kiuchumi

Kupitia mradi huo Jumla ya matofali zaidi ya elfu Thelathini yanategemewa kuzalishwa na kugawanywa maeneo mbalimbali kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo mifuko Mia Sita na Themanini ya Saruji imekwishapokelewa sambamba na Mashine Tano kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa Mwanza kama jitihada za awali za kuanza kwa mradi huo

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
06.06.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com