Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar.
Kama desturi ilivyo viongozi wa Jimbo la Kikwajuni Mbunge na Muakilishi wa Jimbo la Kikwajuni hufanya mashindano ya kuhifadhi qur-an kwa juzuu tofauti mashindano hayo hushirikisha wanafuzi wa vyuo vya qur-an vinavyo patikana ndani ya Jimbo la Kikwajuni.
MH mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Eng: Hamad Yussuf Masuni ambae Pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alisema kuwa Mashindano hayo yanamiaka mitatu sasa tangu kuasisiwa kwake na kwa maandalizi ya mwaka huu yote yamekamilika.
Tunawomba wananchi wote kuhudhuria kwenye mashindano ya kuhifadhi Quran, kusoma tajweed na kaswida yatakayo fanyika siku ya Jumapili tarehe 18/06/2017 saa 2.00 asubuhi kwenye viwanja vya mnara wa Mapinduzi Kisonge Katika Ghafla hiyo pia tutatambulisha rasmin Mfuko wa Elimu wa Jimbo la Kikwajuni *Kikwajuni* *Education *Development Fund* ambao utaanza kutoa huduma za kusaidia na kutatua changamoto za elimu kwa walimu na wanafunzi hususan Mayatima na wasio na uwezo kiuchumi mazingira miundombinu na nyenzo za kusomea na kusomeshea.
MH Masauni Pia alieleza Mambo mbali mbali ya utekelezaji ilani waliofanya ndani ya Jimbo la Kikwajuni alisema sio sekta ya elimu tu hata Michezo hivi karibuni waliazisha Mashindano ya Nage walitoa vifaa mbali mbali vya michezo na FEDHA taslimu kwa vilabu vyote vya ndani ya Jimbo na kwasasa kuna Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayo endelea wakati wa usiku viwanja wa Mnazi Mmoja Mashindano anbao yamefikia hatua ya robo fainali.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Balozi Seif Ali Idi, Makamo wa Pili wa Raisi wa Zanzibar katika Mashindano ya Qur-an siku ya Jumapili hivyo waislamu wote wajitokeze kwa wingi kutakuwa na maswali kwa watazamaji wa mashindano hayo ambayo yataulizwa yanahusu dini ya kiislamu na mshindi atapata zawadi.
0 comments:
Post a Comment