METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 14, 2017

MAKONDA ATEKELEZA AHADI YA KUWAZAWADIA WASHINDI WATANO WA KUHIFADHI QURAN

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda leo ametimiza ahadi yake ya kuwazawadia washindi watano walioshinda katika Mashindano ya Afrika ya kuhifadhi qur-an yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Taifa.

Mhe Makonda amewazawadia washindi 5* kila mmoja kiasi cha shilingi milioni moja fedha taslim za kitanzania.

Katika Makabidhiano hayo Mkuu huyo wa Mkoa amesema " Nimejifunza mambo mengi sanaa siku ile kwani mmeonesha kuwa na nidhamu ya hali ya juu na naahidi mwakani nitakuwa nanyi Bega kwa Bega ili kuhakikisha tunaifanikisha shughuli hii kwa kiwango cha juu zaidi ".

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com