METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 14, 2017

MAKATIBU WA JUMUIYA ZA CCM SHINYANGA WAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Watendaji wa Jumuiya za  chama cha mapinduzi UVCCM, UWT na Wazazi, Wilaya na kata  za  Shinyanga Mjini wamefanya kikao Cha pamoja,  Katika ukumbi wa ofisi ya UVCCM Shinyanga Mjini.

Pamoja na mambo  Mengine yaliyojili katika kikao hicho pia Tumepokea Taarifa ya uchukuaji na urejeshaji wa form ngazi ya kata katika kata zote za wilaya ya Shinyanga Mjini , katika Taarifa iliyowasilisha na Baadhi ya watendaji wa ngazi za kata imeonekana zoezi la Uchukuaji wa Fomu linaendelea vizuri sana.

Katika kikao hicho pia viongozi wa kata wote kwa pamoja walimpongeza Mh.Rais Dr.John Pombe Magufuli kwa utendaji kazi Mzuri na kuwataka viongozi wengine wamuunge Mkono Rais wetu na M/kiti wa chama Cha mapinduzi Taifa kwa Jinsi Ambavyo Amekuwa Mzalendo na Mchapakazi katika Taifa letu la Tanzania, Nae katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Comrade *Hussein Egobano* aliwataka watendaji wa Jumuiya wote wamuunge Mkono Raisi kwa kuelezea yale Mazuri Ayatendayo  Mh.Raisi wetu Mpendwa na kuacha  Baadhi ya wapinzani wasiokuwa na nia njema na Taifa letu , katibu alisema wanaCCM Mtembee vifua mbele kwani ilani yetu ya uchaguzi Inasimamiwa vizuri, na kwa kutambua hilo nanyi pia Muendelee kuwa wazelendo kwa chama chetu, kwa kuwa waadirifu katika uchaguzi huu wa chama kwa kuepuka _Rushwa_, na unyanyasaji wa wanaccm wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali ya Chama ya Chama na Jumuiya zake.

Nae katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Dada Rhoda aliwaomba viongozi kuepuka makundi na kusimama imara ili kukitetea chama na kuacha kupanga safu  , kwani kwa kufanya hivyo itapelekea jina lako kukatwa hata kama utakuwa Umeshinda kwa Kura nyingi.

Pia katibu wa CCM wa wilaya Ndugu Sangura aliwapongeza watendaji wa Jumuiya ngazi ya wilaya na kata kwanamna Ambavyo wanajitoa kufanya kazi za Chama bila kujari Changamoto wanazokutana nazo katika Chaguzi hizi, katibu aliwaambia Mwisho wa uchaguzi mwingine ndio maandalizi ya Uchaguzi Ujao kwahiyo niwatake Muende kuchagua viongozi watakao  Pambana kwa hali na mali kuhakikisha Tunapata Ushindi 2019/2020

Makatibu waliwashukuru viongozi wao wa wilaya kwa namna Ambavyo wamewaasa na kuahidi kutoa Ushirikiano mkubwa ili kufanikisha, chaguzi hizi na zijazo.

Imetolewa na
Katibu wa UVCCM (w)
Shinyanga Mjini.
Comrade Egobano.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com