METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 23, 2017

HUMPHREY POLEPOLE ASHUHUDIA UTEKELEZAJI WA ILANI NA SERA ZA CCM KTK ZIARA YA MH RAIS MAGUFULI MKOA WA PWANI

Na PETRO MAGOTI
Ndg Humphrey Polepole amemaliza ziara ya siku 3 mkoani Pwani iliyoanza tarehe Juni 20, 2017 kwa mafanikio yenye tija lukuki kwa mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla Huku Akiwa Ameambatana na MH RAIS MAGUFULI BAADA ya kumualika KWENDA kuangalia Utekelezaji wa Ilani na Sera ya CCM
Katika ziara hiyo, Mh Rais Magufuli amezindua viwanda vitano ambavyo ni viwanda vya vifungashia, kiwanda cha Matrekta, kiwanda cha chuma, kiwanda cha kukausha matunda na kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona.Hii ikiwa ni Miongoni mwa Utekelezaji wa Sera na Ilani ya CCM 2015/2017
Uzinduzi wa viwanda hivyo ni muendelezo wa kutekeleza ahadi, SERA na Ilani YA CCM aliyoitoa wakati wa uchaguzi mkuu 2015/2020 kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa Tanzania ya viwanda. Viwanda hivyo vitasaidia kuondoa tatizo la ajira nchini na pia vitasaidia kupunguza bei za bidhaa husika kwenye soko la kibiashara.
Serikali ya awamu ya 5 ya Dk. Magufuli inayoongozwa na CHAMA TAWALA CCM ambayo ina miaka 2 tangu iingie madarakani imefanikiwa kupata viwanda 393 ndani ya mkoa wa Pwani ambavyo kati ya hivyo viwanda 85 ni viwanda vikubwa. Hakika Tanzania ya viwanda inawezekana
Rais Magufuli na M/KITI WA CCM na huyo huyo amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha kutengeneza dawa za kuulia vimelea vya mbu wanaosababisha malaria kilichopo Kibaha, Pwani ambapo Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha kutoa Sh1.3 bilioni  kwa ajili ya kulipia lita 100 ya dawa  hizo za kuua vimelea vya mbu zilizopo katika kiwanda hicho.
Wizara inatumia gharama kubwa kununua madawa ya kutibu nje ya nchi na kuacha dawa inayozuia maleria ikikosa mnunuzi hapa nchini. Nina uhakika uamuzi huu wa Rais utasaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa Malaria hapa nchini nayo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sera na Ilani ya CCM.
Katika ziara hiyo, Ndugu Humphrey Polepole akiwa sambamba Mh Rais Magufuli waliendelea kukagua na Kuangalia SERA NA ILANI YA CCM 2015/20 Walizindua Barabara ya Bagamoyo – Msata ambayo imejengwa kwa fedha zetu wenyewe na walioijenga ni wakandarasi wazawa.
Barabara hiyo itasaidia kupunguza foleni ya Barabara ya Dar Kibaha, itaongeza uchaguzi wa njia ya kutoka na kuingia mkoa wa Dar, utasaidia kusafirisha watu na mizigo yao yakiwemo mazao kutoka mashambani na kuyafikisha masokoni kwa gharama ndogo. Hakika Barabara h MAGUFULI Akiwa Shuhuda wa na MSIMAMIZI wa Utekelezaji wa Shughuli za Sera na Ilani ya Chama.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com