Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Bi. Maua Athumani Daud mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa kijiji cha kajima, kata ya jakika, Tarafa ya matemanga wilayani Tunduru ameuawa na tembo. Kumekuwepo na matukio ya tembo kuamia makazi ya watu.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera alikwenda eneo la tukio akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mhe. Mbwana Mkwanda Sudi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tunduru Ndg. Hamisi Kaesa, wawakilishi wa Shirika la World Wide Fund for Nature(WWF) na wawakilishi wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) kanda ya kusini.
Dc Homera alifika eneo la tukio na kuelezwa na Mume wa marehemu Bw. Issa kalolo tukio nzima.
Bw. Kalolo, alisema kuwa mke wake aliondoka nyumbani majira ya saa nne usiku na kwenda shambani kufuata mpunga aliovuna mchana, lakini kwa bahati mbaya alikutana na kundi la tembo na alipo mulika tochi, tembo mmoja alianza kumkimbiza hata hivyo mkewe alifanikiwa kukimbia hadi kufika nyumbani, ndipo alipoanguka na tembo kuanza kumkanyaga hadi umauti ulipomkuta.
Aidha, Dc Homera akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama walienda kuangalia mwili wa marehemu na kushiriki Ibada ya kumuombea marehemu Maua Athumani Daud ambae alizikwa majira ya saa kumi jioni.
Akizungumza na wananchi walio hudhuria msiba huo, Mhe. Homera alisema serikali imeguswa sana na msiba huo na taifa limepoteza nguvu kazi.
Aliendelea kusema, tatizo la tembo sio la Tunduru tu bali ni tatizo la maeneo yote yanayo zungukwa na hifadhi.
Hata hivyo DC Homera alisema kutokana na madhara ya tembo kijijini hapo, alieleza kwamba atalifanyia kazi ombi la kurejeshewa silaha iliyochukuliwa na jeshi la polisi, silaha iliyokuwa inamilikiwa na kijiji kupitia kikundi cha vijana 10 kilichoundwa chini ya NALIKA kikosi cha kulinda tembo na raia.
Katika hatua nyingine DC Homera alisema huu ni muda muhafaka kwa serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii kuja na njia mbadala ya kuwafukuza tembo kwenye mashamba ya watu, njia ya kienyeji ya kuweka pilipili, majivu pamoja na mizinga ya nyuki imekuwa na changamoto nyingi.
Mwishoni, DC Homera aliwaomba wananchi waanze kulima pamoja ili iwe rahisi kulinda mazao, sasa hivi kila mtu anajilimia kwake hivyo tembo akifukuzwa kwenye Shamba la mtu mmoja anakimbilia kwenye Shamba la mtu mwingine.
0 comments:
Post a Comment