METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 20, 2017

KAIMU NAIBU KATIBU MKUU UVCCM ZNZ AWAKUTANISHA VIONGOZI WA UVCCM NA VIONGOZI SHIRIKISHO ZNZ

Na mwandishi Wetu, Zanzibar

Mh Abdullghafar Idirissa Juma Kaimu Naibu Katibu Mkuu UVCC Zanzibar leo alikutana na watendaji wa UVCCM ngazi ya Wilaya na Mikoa kwa pamoja na Viongozi wa Shirikisho kwa matawi yote ya Vyuo vikuu ZNZ pamoja na viongozi wakuu wa shirikisho kwa upande wa Zanzibar.

Katika kikao hicho Kaimu Naibu alisema ameitisha kikao hicho ili viongozi wa lililokuwa shirikisho na viongozi wa UVCCM wapate kujuana ili wafanye kazi pamoja.

*Awali vyuo vikuu walikuwa na Shirikisho hivyo walikuwa wakijitegemea vitu vingi kwa sasa kutokana na Katiba mpya na Kanuni mpya ya UVCCM Shirikisho kimefutwa rasmin na kuwa idara ndani ya UVCCM hivyo nilazima tufanyekazi kwa pamoja*

Tumeitana kukumbusha muongozo chaguzi zinaendekea kwa upande wa UVCCM ila muongozo wa idara ya vyuo na ratiba ya chaguzi za matawi ya vyuo zimetoka hivyo kwa pamoja tushirikiane ili kukamilisha chaguzi hizo alisema Abdullghafar.

Nao viongozi wa UVCCM na wa Vyuo walimpongeza Kaimu Naibu kwa kuwakutanisha na kuwakumbusha kuwa wao ni wamoja wanatafautiana mipaka na maeneo ya kazi ila lengo ni moja hivyo wameahidi kushirikiana bega kwa bega ili kufikia malengo ya kuipata CCM MPYA TANZANIA MPYA

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com