METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 20, 2017

SALAMU ZA DC JUMA HOMERA KWA MAKADA WANAOHITIMU VYUO VIKUU MOROGORO

Na Mwandishi Wetu, Tunduru

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera aliwasili katika ukumbi wa usambala hoteli iliyopo morogoro mjini kwa mwaliko wa Makada wanao hitimu vyuo vikuu toka vyuo mbali mbali mkoani humo, Dc Homera alizungumza na makada hao wakati wakimsubiria mgeni rasmi wa sherehe hiyo  Mhe. Antony Peter Mavunde (MB) Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.

DC Homera aliwasihi vijana hao

1. Wakipigania Chama Cha Mapinduzi kwa hali na mali katika kuhakikisha kinaendelea kushika hatamu na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi 2015-2020.

2. Wawe wavumilivu kwani ni kipimo cha uzalendo ndani ya nchi na chama chetu kwa ujumla.

3. Wajitokeze kugombea nafasi mbali mbali huko waendako na wakajitambulishe kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo wanayotoka au Mikoa na Wilaya.

4. Waunge mkono jitihada za viongozi wa chama ngazi zote katika kuunda mashina yenye wanachama 150 na zaidi.

5. Wapendane kama wana CCM ili kuendelea kudumisha umoja na mshikamo katika chama chetu.

Aidha, Dc Homera alichangia mfuko wa wana Vyuo Morogoro shilingi laki mbili.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com