METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, May 18, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AKAGUA MIUNDOMBINU YA AFYA NA MADARAJA

Na Ofisi Ya Mbunge, Ilemela

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amefanya ziara ya ufuatiliaji na ukaguzi wa miundombinu ya hospitali ya Buzuruga na kukagua ukarabati wa jengo hilo unaoendelea, ukarabati wa barabara kale ya Sangabuye-Buswelu na madaraja ya kata ya Mecco kwa kutumia fedha za mfuko wa Jimbo na Manispaa ya Ilemela ikiwa ni hatua katika ufumbuzi wa changamoto na adha zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe Mabula amesema kuwa amedhamiria kuhakikisha anatatua changamoto zote zinazowakabili wananchi wake pamoja na majukumu ya kitaifa aliyonayo na ziara hiyo ni hatua katika kuhakikisha anatekeleza kwa vitendo alichokidhamiria

‘… Tumedhamiria kuhakikisha kuwa tunatekeleza kwa vitendo adhma ya kumaliza kama si kupunguza kero na changamoto zinazowakabili wananchi wetu na kupitia ziara hii tunatafsiri kile tunachokizungumza kama Ilani yetu ya uchaguzi inavyoelekeza …’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Jimbo lake kuendelea kumpa ushirikiano na kuwajibika ili kuyafikia maendeleo wanayoyataka

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buzuruga aliyeambatana na Mbunge  Mhe Richard Machemba mbali na kumshukuru na kumpongeza kwa namna anavyowatumikia wananchi wake bila kujali tofauti zao amemuhakikishia ushirikiano na kumuomba kuzidi kuisaidia kata yake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
18.05.2017

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com