METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, May 18, 2017

MADIWANI WA MANISPAA YA ILEMELA WAMTEMBELEA MBUNGE WAO DKT ANGELINE MABULA MJINI DODOMA

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamepata fursa ya kumtembelea Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mjini Dodoma wakiambatana na baadhi ya wataalamu wa Manispaa hiyo wakiwa njiani kuelekea mjini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi katika kujifunza mambo mbalimbali ya kiuchumi na uwekezaji katika kituo cha  EPZ

Akizungumza na madiwani hao Mhe Angeline Mabula amewataka madiwani hao kuitumia vizuri fursa ya mafunzo kwa kuzingatia watachojifunza ili kilete tija na maslahi mapana kwa wananchi wa Ilemela.

' Niwatakie kila la kheri katika safari yenu hii ya mafunzo kuelekea  Jijini Dar es Salaam lakini niwaombe sana mkazingatie mafunzo ili kuleta tija na maslahi mapana kwa wananchi wetu '

Kwa upande wao madiwani hao wakiongozwa na Mhe Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga wamemshukuru Mbunge wao kwa namna anavyounga mkono na kujitoa katika kuwaletea wananchi wake maendeleo huku wakimuahidi kutumia nguvu na maarifa yao yote kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa na tija na maslahi mapana kwa wananchi wa Ilemela.

'' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ''

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
19.05.2017

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com