Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Tigo, Aidan Komba, akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mkoani Singida, kushoto ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Singida Raymond Royer.
Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma ya 4G LTE mkoani singida mapema leo.
Wateja wa Tigo mkoani Singida
hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi
kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo
uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara
tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika
soko.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo
Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo
unafuatia mafanikio yaliyopatikana baada ya kuizindua katika mji mingine
mikubwa nchini.
Komba alisema kwa kuifanya
huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo kwa mara nyingine tena imeonesha
kujikita kwake katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya
kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu
katika soko hili.”
Alitangaza kuanza kwa enzi
mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano ndani ya Singida
akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha kunakuwepo uwezo mkubwa na
muhimu katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.
“Singida ni kituo muhimu
kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba
wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia huduma
Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa
rahisi zaidi.”
“Mawasiliano ya simu ni nguzo
muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika
maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na
hali kadhalika kukuza uchumi na biashara”, alisema Komba.
“Kama mnavyojua, Tigo imekuwa
mstari wa mbele katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri
ukiwa ni uchimbaji wa visima 12 ambavyo tulivitoa kama msaada kwa vijiji
vya Singida mwaka jana,” Komba alibainisha.
Aliongeza kwamba gharama ya
vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua
kuwa wateja wanachotakiwa ni kuwa na kifaa kinachowezesha 4G LTE ama
simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE
ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja
wanaweza kubadilisha au kununua kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika
duka la Tigo la huduma kwa wateja lililopo Singida Mjini.
Akizungumzia uwekezaji katika
mtandao, Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika
miundombinu ya kisasa, ikilenga kusaidia katika maendeleo endelevu ndani
ya mkoa.
Alihitimisha kwa kusema,
“Mipango imo njiani katika kupanua huduma kwa ajili ya mikoa iliyobakia
ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”
Kwa upande wake, Meneja wa
mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer alibainisha umuhimu wa
huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha huduma za uwanda mpana wa
simu za mkononi.
Royer alisema, “Katika kipindi
cha hivi karibuni kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja
na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia
90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”
Aliongeza, “Kwa hiyo
teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za data zilizo na
kasi kubwa na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko ambayo
itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”
Mtandao wa 4G LTE unamaanisha
kasi kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada kutoka katika
intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango
kikubwa inaboresha uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya
mikutano. Hali kadhalika inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano
wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na
kutiririsha video kutoka katika mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment