- Imeandikwa na Isdory Kitunda
- MKAZI wa Kijiji cha Nyarero, tarafa ya Inchage, wilayani Tarime,
mkoani Mara, Magita Enoshi (50) amehukumiwa kwenda jela maisha baada ya
kupatikana na hatia ya kushambulia kwa mapanga na kumkatakata jirani
yake, John Kichere sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia ulemavu
wa maisha.
Akisomewa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Joaquine De-Mello alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali, Harry Mbogoro.
Awali ilidaiwa kuwa mtuhumiwa Enoshi, mnamo Oktoba 20, mwaka 2010 saa moja jioni kwa nia mbaya ya chuki akiwa na panga alimshambulia Kichere ambaye ni jirani yake kwa kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo mkono na kukatika vidole vitatu, kumkata shingoni na mgongoni na kumsababishia majeraha makubwa na kupoteza fahamu kwa muda.
Ilidaiwa kuwa baada ya kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu yaliyochukuwa muda mrefu kupata nafuu, sasa majeruhi amepata ulemavu wa kudumu. Awali mtuhumiwa huyo alikana shitaka hilo na upande wa utetezi wake ukiongozwa na wakili wa kijitegemea, Msafiri Henga alidai kuwa mlalamiko ya Kichere dhidi ya mteja wake, Enoshi yalikuwa ya chuki. Hata hivyo, kutokana na ushahidi, Jaji De-Mello alisema imedhihirisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo. “Ninakuhukumu kwenda jela maisha ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbovu ya kuwadhuru wenzao,” alisema Jaji De-Mello.
Tuesday, May 16, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment