METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, April 14, 2017

RC MAKONDA ASEMA RAIS MAGUFULI ATAZINDUA MABWENI NA UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA ZA (NHC) MAGOMENI KOTA

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kesho Jumamosi April 15, 2017 kuanzia majira ya saa tatu asubuhi anataraji kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Mara baada ya kutembelea eneo la UDSM kufanya ukaguzi wa maandalizi ya dhifa ya hapo kesho, alisema kuwa Mara baada ya uzinduzi huo Rais Magufuli pia ataelekea katika Mtaa wa Magomeni ambapo ataweka Jiwe la Msingi
Ujenzi wa nyumba za serikali (NHC) alizowaahidi wananchi waliokuwa wamepoteza matumaini ambapo watapata fursa ya kuishi Bure.

Rc Makonda alisema kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) waliokuwa wanapata shida mitaani kwa kupata adha kubwa ya Malazi kwa kuishi katika mazingira magumu na hatarishi yasiyoweza kuwapa fursa ya kusoma na kufaulu vizuri sasa watapata ahueni baada ya kukamilika kwa Mabweni hayo ambayo yatatoa unafuu kwa Kila mwanafunzi.

Alisema kuwa zaidi ya wanafunzi 3840 watapata fursa ya kuishi kwa amani pasina mashaka ya malipo kwani katika kipindi cha Semista nzima watatumia gharama ya Shilingi Laki moja na elfu kumi pekee (110,000) tofauti na gharama kubwa za mitaani ambazo walikuwa wanalipa zinazokaribia shilingi milioni moja kwa Semista moja.

Alisema kuwa hali ya maisha ya mtaani kwa wanafunzi wengi wa Chuo hicho ilikuwa ni ngumu sana jambo ambalo lilikuwa linawapa vishawishi wanafunzi wengi kuingia na kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya kwa kuamini kuwa wanapunguza Mawazo yanayowakabili kutokana na ukata wa maisha.

Rc Makonda ameeleza kuwa Rais Magufuli ni kiongozi aliyeletwa na Mungu kwa ajili ya watanzania ambaye anaonekana kwa matendo na kauli zake jinsi ambavyo anawatetea watanzania wanyonge na masikini.

"Rais akisema anatenda, Akisema anatekeleza, Na akiahidi anatekeleza, Hivyo ni wajibu wetu kumuombea kwa Mungu na kumtia Moyo ili aifanye kazi tuliyomkabidhi ya kuwapigania watanzania wanyonge na Masikini" Alisema Rc Makonda

Octoba 21, 2016 Rais Magufuli aliweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Mabweni 20 ya wanafunzi 3840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi June 2016 wakati wa uzinduzi Maktaba ya Kisasa ya Chuo hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com