METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 12, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MGENI RASMI MAOMBEZI YA AMANI NCHINI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ashiriki maombezi ya kuliombea Taifa na Viongozi wake wote katika Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli yaliyofanyika katika Viwanja vya Ccm Kirumba na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali.

Aidha katika kongamano hilo lililoandaliwa na akina mama wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza lilidumu kwa muda wa siku tatu ambapo mbali na kuombea Taifa limezungumzia changamoto mbalimbali anazokumbana nazo Mwanamke,  Mmomonyoko wa maadili kwa Vijana,  Namna ya kumkomboa Mwanamke kiuchumi,  Tatizo la Ajira kwa Vijana, na Nafasi ya Mwanamke katika kulisaidia Taifa.

Akizungumza katika kongamano hilo Dkt Mabula amewataka Wanawake wote nchini kujisimamia katika kulisaidia taifa sambamba na kuacha utegemezi kwa kuthubutu na kuchukua hatua katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa upande wao wanawake walioshiriki kongamano hilo mbali nakumshukuru Mhe Dkt Mabula kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa Mgeni rasmi katika kuhitimisha kilele cha kongamano hilo wamemhakikishia kuwa Wanawake wataendelea kuwa msingi imara katika kuliletea Taifa maendeleo hasa kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya Viwanda huku Mwanamke akitegemewa kama nyenzo muhimu na chachu ya kuyafikia malengo hayo kwa kujituma na kuacha utegemezi na mwisho kumkabidhi zawadi ya picha kwa niaba ya Mhe Janeth Magufuli mke wa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ishara ya kuthamini na kuutambua mchango wake kama mwanamke katika kulitumikia Taifa na Msaidizi mahiri wa Mhe Rais.

' Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
12. 04. 2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com