Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta
Kabati aliongea neono wakati wa harambee ya kuchangia fedha za kununulia
gari kwa ajili ya maendeleo ya UKWATA
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta
Kabati akiwa na viongozi mbalimbali waliokuwepo wakati wa harambee ya
utafutaji wa kupata Pesa za kununulia gawa ajili ya UKWATA Mkoa wa
Iringa.
Baadhi ya wanaukwata waliokuwepo siku ya harambee kutoka maeneo mbalimbali Mkoani iringa
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati amechangia ushirika wa
Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) iliyo chini ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT) inayolenga kuwasaidia Wanafunzi wa Madhehebu ya
CCT kiroho na kimaadili katika shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi ,Vyuo
vya Elimu na Vyuo vingine vya Kanisa na vya Serikali kwa ajili wa
kununua basi ambalo liatakuwa linagharimu Zaidi ya million sitini.
Akizungumza
wakati wa harambee ya kutafuta Pesa za kununulia gari Mbunge Kabati
alisema kuwa jamii ya kikristo inapaswa kuendelea kuwa wamoja ili
kuendelea kudumisha umoja wa watanzania kwa kuwa UKWATA ni sehemu ambayo
inawafundisha maadili wanafunzi ya jinsi gani ya kuishi kwa umoja na
kumuabudu mungu.
"Saizi
tuna vijana wengi wapo mitaani hawamjui mungu na wamekuwa wanatumia
madawa ya kulevya,wengine wanatumika katika kazi za kishetani kwa kuwa
wengi wao hawakupata mafunzo kutoka kanisani au msikitini hiyo viongozi
na walezi wa UKWATA lazima muwekeze nguvu za kutosha ili kuikomboa jamii
yetu ya kitanzania"alisema Kabati
Kabati
aliwataka vijana kukua katika maadili ya kimungu kwa kuwa ndio malezi
mazuri kwa mwanadamu yoyote yule hivyo tunatakiwa kuwashauri vijana
wengi wanapotea kwa kuwa hao wote ni lika yenu na mnaishi na kucheza
pamoja.
Suluhisho
la changamoto zinazowakabili Vijana ni kama jamii na wadau mbalimbali
wa Maendeleo kama serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserekali ( NGO’s),
Kanisa na Vijana wenyewe wataweza kuona changamoto hizi na matokeo yake
kisha kufikiri njia za kukabiliana nazo.
Vijana
wakitambuliwa, wakihamasishwa, kuwezeshwa na kupewa elimu na maadili
bora katika maeneo yote na nyanja zote, tatizo litapungua kama si kwisha
kabisa. Wachungaji na wote wanaopenda maendeleo ya Vijana wanao wajibu
wa kuhimiza Uinjilisti kwa vijana, huduma ya ushauri na utunzaji hali
kadhalika kutenga muda wa Neno na Maombi na Vijana ikiwezekana mara moja
kwa mwezi itasaidia sana kupunguza tatizo.
Kwa
baadhi ya walezi walikuwepo katika harambee hiyo walimpongeza na
kumshukuru Mbunge Kabati kwa jitihada anazozifanya kuisadia jamii kwa
kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa Mkoani iringa na Tanzania
kwa ujumla.
Lakini
walezi hao wa UKWATA waliomuomb mbunge huyo kuwasidia kufanikisha lengo
lao la kununua gari aina ya basi hata kwa kuwaombea kwa wabunge na
viongozi wengine kwa kuwa uwezo huo anao.
"Leo
mbunge Kabati ametuchangia shilingi million moja kwa hiyo tukienda kwa
viongozi wengine najua tutapata Zaidi kwa kuwa yeye pia ni Mwenyekiti wa
wabunge wote wa Mkoa wa Iringa hivyo itakuwa njia rahisi kutufanikishia
adhima yetu hata hivyo tunamshukuru kwa kuwa nilikuwa ghafla sana ila
amekuja na katuchangia tunamshukuru na tu naomba mungu ambariki katika
kazi zake" walisema walezi wa UKWATA mkoa wa Iringa.
Nao
baadhi ya viongozi wa UKWATA Mkoa wa Iringa walisema kuwa Malengo Makuu
ya UKWATA ni kuwasaidia Wanafunzi wawe na msingi bora wa maisha ya
kiroho kwa njia za Ibada za pamoja,Vipindi vya kujifunza Biblia, Maombi,
Sala. Chini ya UKWATA, Vijana Mashuleni huimarishwa kuiga tabia ya Yesu
Kristo katika kudumisha Umoja, kuhudumiana kiroho na kimwili wao kwa
wao, pia kuwa na maandalio ya Kikristo na kutiwa moyo katika kulitumikia
Kanisa.
Viongozi
wa UKWATA walimshukuru mbunge Kabati kwa kuwa changia kiasi cha fedha
ambazo zinawafanya waamini kuwa siku moja watatiza malengo yao ya
kununua basi ambalo kitakuwa msaada kwao na kuondokana na kuwa omba
omba.
0 comments:
Post a Comment