METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 11, 2017

MAGUFULI AMWAGA VITANDA VYA WAGONJWA NCHI NZIMA

Na Mwandiahi Wetu, Dodoma

Katika Muendelezo wa Utekelezaji wa Ahadi za Mh Rais Magufuli Kusambaza Vitanda Nchi Nzima katika Vituo vya Afya.

Wizara ya Afya ilitenga Tsh 4,000,000,000,00 katika Bajeti ya Mwaka 2016/2017, Sasa Wizara imeanza utekelezaji Huo kwa Halmashauri zote 184 Nchini.

Uzinduzi wa Zoezi hilo Umefanyika Leo 11/04/2017  katika Halmashari ya Kongwa, Ambapo Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu Amemkabidhi Mh Job Ndugai Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu ya Vifaa hivyo.

Katika Zoezo hilo kila Halmashauri nchini itapatiwa Vitanda vya Hospitali vya Kawaida (Hospital Beds) 20; Vitanda vya Kujifungulia wajawazito (Delivery beds) 5;
Magodoro 25 na Mashuka 50.

Jumla ya Vifaa vitakavyogawiwa Halmashauri zote 184 nchini ni Vitanda vya Hospitali vya Kawaida (Hospital Beds) (3,680); Vitanda vya Kujifungulia Wajawazito (Delivery Beds) (920); Magodoro (4,600); na Mashuka (9,200).

Thamani ya Vifaa hivi ni Tsh Billion 2,933,125,600. Zoezi hili linatarajiwa kukamilika kabla ya Tarehe 30 June 2017.

Aidha Awamu ya pili ya Mgawo huu itahusisha Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali Maalum. Ni Matarajio ya Wizara kuona vifaa hivi vinagawiwa kwenye Vituo vya kutolea Huduma za Afya vya Umma vyenye uhitaji kwa kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri Husika.

Wizara ya Afya inapenda Kumshukuru Mh Rais Magufuli kwa Uwamuzi wake wa kuhakikisha fedha za Umma zinatumika kwa Ajili ya Kuboresha Huduma za Afya hapa Nchini.

Ameyasema nakufafanua vyema waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu aliwa Kongwa ktk Ugawaji wa Vifaa Hivyo.

KWA PAMOJA, TUNABORESHA AFYA ZETU!

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com