METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 11, 2017

KAMATI YA MAANDALIZI YA MITIHANI MKOA WA DAR ES SALAAM YAKAGUA MAPENDEKEZO YA KAMATI YA NGAZI YA MANISPAA YA UBUNGO MAHALA PA KUHIFADHI MITIHANI YA KIDATO CHA SITA

Mwenyekiti wa KAMATI ya Maandalizi ya Mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2017 ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Ndg Khamis Lissu (Kulia) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kamati ya Uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa Kidato cha Sita Mwaka 2017 na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2017 wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita
Mwenyekiti wa kamati ya Uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Kibamba wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita

Mwenyekiti wa KAMATI ya Maandalizi ya Mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2017 ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Ndg Khamis Lissu (Mbele) akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Nyuma) wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita katika shule ya Msingi Mbezi Luis
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa Kidato cha Sita Mwaka 2017 na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2017 wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita katikasule ya Sekondari Kibamba

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa Kidato cha Sita Mwaka 2017 na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2017 wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita katikasule ya Sekondari Kibamba
Mwenyekiti wa Kamati ya uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo marabaada ya ukaguzi wa eneo la kutunzia mitihani
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa Kidato cha Sita Mwaka 2017 na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2017 wakati wa ukaguzi wa eneo mahususi kwa ajili ya kutunzia Mitihani ya kidao cha sita katikasule ya Sekondari Kibamba

Na Mathias Canal, Dar es salaam

KAMATI ya Maandalizi ya Mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2017 Imekagua mahala pendekezwa na kamati ya Uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo kwa ajili ya kuhifadhia mitihani ya Kidato cha sita inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Tano.

Kamati hiyo ya Mkoa wa Dar es salaam iliyoongozwa na Katibu wake ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Ndg Khamis Lissu imezuru katika maeneo mawili pendekezwa ambayo ni shule ya Msingi Mbezi Luis na Shule ya Sekondari Kibamba na kupendekeza utunzaji wa mitihani kufanyika katika shule ya Sekondari Kibamba.

Ukaguzi huo wa chumba madhubuti kitakachohifadhiwa mitihani ya Kidato cha sita mwaka 2017 umefanyika kwa dhamira ya kutambua sehemu salama na madhubuti kwa utunzaji wa mitihani hiyo kabla ya kuanza kuisambaza katika shule zingine kwa ajili ya wanafunzi kufanya mitihani hiyo.

Katika ziara hiyo kamati ya uendeshaji mitihani Ngazi ya Wilaya iliyoongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo imekaguliwa na hatimaye kupatikana mapendekezo ya Kamati ya Mkoa wa Dar es salaam kuhifadhi mitihani hiyo katika Shule ya Sekondari Kibamba.

Aidha kesho Machi, 12, 2017 kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa kidato cha sita Ngazi ya Mkoa ittakuwa na kikao cha kamati za Maandalizi kutoka Manispaa Zote Tano za Mkoa wa Dar es salaam ili kupokea taarifa ya Maandalizi Na jinsi Manispaa zote zilivyojipanga kwa ajili ya Semina kwa wasimakizi wote wa mitihani Na Maandalizi ya Mitihani.

Katika kikao hicho Kila Manispaa itatoa taarifa yake ya jinsi ilivyo jipanga lakini zaidi zitatazamwa Manispaa mbili ambazo ni mpya ikiwemo Manispaa ya Ubungo na Manispaa ya Kigamboni.

Akizungumza Mara baada ya kukaguliwa Mwenyekiti wa Kamati ya uendeshaji Mitihani Ngazi ya Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imejipanga vyema kuwa na eneo imara na madhubuti kwa ajili ya kutunzia mitihani hiyo ili iwe salama wakati wote katika kipindi cha mitihani.

Kamati ya Maandalizi ya Mtihani wa Kidato cha Sita Mwaka 2017 ina jumla ya watu saba ambapo kamati ya Uendeshaji mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2017 NGAZI ya Wilaya ya Ubungo nayo pia ina watu saba.

Mtihani wa Taifa kwa kidato cha sita unataraji kuanza kufanyika tarehe 2 mwezi ujao na kumalizika April 18 2017 kote nchini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com