METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 11, 2017

KAMATI YA UKIMWI MANISPAA YA UBUNGO YATEMBELEA HOSPITALI YA SINZA

Na Nasri Bakari, Dar es Salaam

Kamati ya Ukimwi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imetembelea na kujionea huduma na matibabu yanayotolewa kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi VVU/HIV katika hospitali ya Wilaya Sinza.

Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh. Ramadhani Kwangaya imefanya ziara hiyo leo katika vitengo vya Ukimwi na kifua kikuu katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara  Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Crispin Kayola alisema anamshukuru Mkurugenzi wa  Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma katika hospitalini hapo zinakuwa nzuri.

Pia aliishukuru kamati hiyo kwa kitendo cha kutembelea katika hospitali hiyo na kujionea utendaji kazi wa wahudumu.

"Kwa niaba ya wahudumu wa hospitali ya Sinza  naishukuru kamati nzima ya Ukimwi kwa kututembelea, kwa mwaka tunahudumia wagonjwa takribani 12597 katika kitengo cha Ukimwi idadi hii inajumuisha 346 kutoka idara ya wajawazito na 65 kutoka idara ya kifua kikuu" alisema Dkt. Crispin na kuendelea;-

"Idadi hiyo ya wagonjwa ni kubwa kulinganisha na miundombinu yetu, tunaomba mlishughulikie hili" alisema Dkt. Crispin.

Wakati huo huo akizungumza baada ya ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Ukimwi Mh. Leila Hussein Madidi amesema amefurahi kuona huduma nzuri zinazotolewa katika hospitali hiyo licha ya changamoto zinazowakabili.

"Nawapongeza wahudumu wa hospitali hii kwa kufanya kazi kwa bidii licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali" alisema Mh. Leila na kuendelea.

"Manispaa ya Ubungo imeziona changamoto hizo na tutazishughulikia" alisema Mhe Leila.

Imetolewa na

Kitengo cha Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com