Leo tarehe 13 Aprili, 2017, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP amekabidhiwa _Cheti cha Pongezi_ kilichotolewa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).
Aliyekabidhi Cheti hicho cha Pongezi ni Ndg.Muhammad Shaban (Aluta.D) ambaye ni Mshauri Msaidizi wa Mwenyekiti-AWAMATA Taifa _kwa niaba ya_ *Chief Daudi Mrindoko* ambaye ni Mwenyekiti-Taifa wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).
Pia tumekabidhi vyeti vingine kwa wapiganaji wafuatao;
Mhe.Zauda Mohamed
(Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa Kilimanjaro)
Mhe.Nuru Selemani
(Mkuu wa Usalama Mkoa Arusha)
Insp Peter Mizambwa
(Afisa Oparesheni Usalama Barabarani Mkoa Kilimanjaro)
Insp Raphael Ganchra
(Vehicle Incharge Mwanza)
Insp Ibrahim Omary Samwix
(Mkaguzi wa Magari Kituo Kikuu cha Mabus Ubungo)
Awali kabla ya kumkabidhi Cheti hicho, alifikisha salamu na pole kwa Kamanda kwa msiba aliopata na pia kuomba dua kwaajili ya marehemu.
Hafla hiyo fupi ilifanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani.
AWAMATA imetambua mchango mkubwa wa *Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP* katika kupungaza ajali nchini na kudhibiti madereva wazembe na pia uongozi mzuri wake mpaka kuanzishwa kwa ulipaji wa faini kwa njia ya kielektroniki na pia kuanzisha Speed Radars ambazo kwa kiasi kikubwa zimeanza kuleta heshima barabarani.
Muhammad Shaban (Aluta.D)
13.04.2017
0 comments:
Post a Comment