METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 13, 2017

AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM ZAZIDI KUKAMILIKA

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Katika kutimizwa kile kinachoitwa Deni la serikali ya Mkoa kwa wakazi wake wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Kinamama ya Chanika unaofadhiliwa na ubalozi wa Korea Kusini na kugharimu zaidi ya Tshs. 8.8 Bilioni za kitanzania uliokamilika  kwa 90% hadi hivi sasa.

Ujenzi huo ambao ulizinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi  na Mh Paul Makonda mwishoni mwa mwaka jana baada ya ombi la ujenzi wa Hospitali ya kisasa kwa wamama wakazi wa Dar es salaam kupokelewa na kukubaliwa na ubalozi wa Korea kusini hapa nchini.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu unasindikizwa pia na ujenzi wa nyumba 28 za makazi kwa ajili ya wauguzi na madaktari watakaohudumu hospitali hiyo masaa 24.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu ambao hadi sasa umebakiza hatua ya mwisho ya ufungaji wa vitanda 160 vya wagonjwa na 10 vya kujifungulia wakina mama wajawazito  (ambayo ni 10% ya mradi wote), ni uthibitisho tosha wa kuonesha nia ya dhati ya Serikali ya Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha huduma bora za kiafya zinawafikia wananchi wote wa Tanzania kwa wakati.

Hospitali hii ya kihistoria na aina yake itakuwa ni mahusisi kwa wakina mama wa Mkoa wa Dar es salaam na wamama wote wa maeneo jirani na inatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh rais wa JMT DrJohn Pombe Magufuli.

Pongezi nyingi zimfikie Mh Paul Makonda kwa jitihada za kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Dar es salaam kwa kishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini.
Kwa Makonda,Mungu atupe nini?

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com