Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma Bodi ya Ununuzi na Ugavi(PSPTB) akitoa mada leo kwa wanafunzi wa Ununuzi na Ugavi katika Chuo cha (IPS) kilichopo Chanika jijini Dar es salaam. wakati wataalamu wa bodi hiyo walipotoa mafunzo ya taaluma hiyo katika chuo hicho, Bw. Ally Songoro amehimiza kufuatwa kwa maadili wakati wa kutekeleza majukumu yao ambapo unatakiwa umakini mkubwa huku wakifuata maadili, Kanuni na taratibu za ununuzi na ugavi wakati watakapokuwa katika ajira zao kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini na kwingineko.
Baadhi ya wanafunzi hao wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu kutoka Bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB) kwenye chuo hicho leo.
Mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho akiwaeleza jambo wanafunzi hao wakati alipokuwa akiwakaribisha wataalamu kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ili kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao.
Shamim Mdee Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma(PSPTB) akizungumza jambo na wanafunzi wa taaluma ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha (IPS) Chanika jijini Dar es salaam.
Shamim Mdee Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma (PSPTB) katikati, Amos Kazinza Afisa Mkuu wa Ushauri na Utafiti (PSPTB) kulia na Jeremiah Haule Afisa Mkuu Mratibu wa Mitaala ya Bodi wakifuatilia mafunzo hayo.
Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma (PSPTB) na Shamim Mdee Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma (PSPTB) wakimsikiliza mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho hayupo pichani baada ya kuwasili chuoni hapo
Amos Kazinza Afisa Mkuu wa Ushauri na Utafiti (PSPTB) kulia, Jeremiah Haule Afisa Mkuu Mratibu wa Mitaala ya Bodi katikati na Philberth Philipo Rais wa Shirikisho la wanafunzi wa kozi ya Ununuzi na Ugavi Vyuo Vikuu vya Tanzania wakiwa katika ofisi ya mkuu wa chuo hicho baada ya kuwasili chuoni hapo.
Wanafunzi hao wakifuatilia mada katika mafunzi hayo.
Amos Kazinza Afisa Mkuu wa Ushauri na Utafiti PSPTB akitoa mada kwa wanafunzi hao.
0 comments:
Post a Comment