METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 27, 2017

SIMBACHAWENE: KAMPENI YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NI AJENDA YA KUDUMU

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri wakati wa kikao kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, na Wakurugenzi wa Halmashauri wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene wakati wa kikao kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri wakati wa kikao kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene wakati wa kikao kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. makonda akielezea jambo wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisisitiza jambo wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, na Wakurugenzi wa Halmashauri wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene wakati wa kikao kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akielezea jambo wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amosi Mkala akizungumza wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma
Mkurugenzi wa Jiji la mwanza Ndg Kiomoni Kibamba akiuliza swal wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 tarehe 27/03/2017 Ukumbi wa Hazina-Dodoma

Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali imejipanga kuendelea kuwabaini watumiaji, Wasafirishaji na Wauzaji wa Dawa za Kulevya na kuwachukulia hatua stahiki ambapo imeeleza kuwa Vita dhidi ya kupambana na Dawa za kulevya nchini inapaswa kuwa Agenda ya kudumu kwa kubaini Dawa hizo zinazozalishwa viwandani zikiwemo Heroin na Cocaine pamoja na zile zinazolimwa ambazo ni Bangi na Mirungi.

Hayo yamebainishwa na waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene wakati wa Kikao cha kazi na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kwa ajili ya uwasilishaji wa mapendekezo ya mipango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

Simbachawene amesema kuwa Dawa za Kulevya zimekuwa janga kubwa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa ambao ni vijana hivyo ili kuimarisha utendaji kazi na kufikia uchumi wa kati ni lazima serikali isimamie na kuhakikisha inateketeza Dawa za kulevya nchini.

Alisema kuwa Wakuu wa Mikoa wanapaswa kuwasaidia Wakurugenzi kuliko kuwalaumu kwani wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na ofisi zao kuwa na matakwa ya kisiasa.

Simbachawene alisema kuwa Bajeti zinatakiwa kuandaliwa kwa kulenga kutatua kero za wananchi ili ziwe na majibu kwao walau kwa asilimia 40% kwa mwaka.

"Nawasihi sana kutumia mifumo bora ya ukusanyaji kodi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki pamoja na kusimamia vyema mapato na matumizi ya ndani" Alisema Simbachawene

Hata hivyo amewapongeza Wakuu wa Mikoa wanaofanya makongamano ya fursa za uwekezaji kwa kutangaza mikoa yao kwa kuelezea fursa na mafaniko yaliyopo sambamba na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuwekeza.

"Mnapaswa kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuzalisha zaidi kwani kufanya hivyo kutatoa ajira za kutosha na kutoa hamasa ya uwekezaji.

Sambamba na hayo pia Mhe Simbachawene ameelezea mipaka ya utendaji kati ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na watumishi wengine kuwa ni pamoja na ruksa waliyonayo Wakuu hao ya kuwaweka watu ndani kwa makosa mbalimbali ya uvunjifu wa Amani au wanaodhaniwa kufanya makosa ya jinai.

Alisema kuwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwaweka watu ndani kwa makosa mbalimbali si chuki bali ni utaratibu wa kisheria japo hawapaswi kutumia mamlaka hayo kinyume na utaratibu.

Miongoni mwa mambo yaliyopewa msisitizo zaidi ni pamoja na Uzalishaji wa madeni, Kupambana na Ongezeko la vifo vya kina mama wajawazito na watoto, Upotevu wa Dawa katika vituo vya kutolea huduma, Fedha za mfuko wa pamoja wa afya, na Kampeni ya Dawa za kulevya.

Msisitizo mwingine ni kuhusu Kuundwa kwa kamati za mikoa za watu wenye ulemavu, TAKUKURU Kutowekwa kwenye kamati za uchunguzi, Fedha za OC kwenda haraka kwa makatibu wa Wilaya kama zilivyokusudiwa pamoja na Uadilifu na Nidhamu.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com