Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2017 amefanya ziara katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mburahati ili kujionea hali ya utendaji kazi katika kata hiyo sambamba na Kubaini changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi Kayombo amefanya kikao na baadhi ya watumishi wanaohudumu katika Kata hiyo ambapo pia amefanya kikao na Madalali wa Soko la Mburahati ambapo wameeleza changamoto zao katika uwajibikaji.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Kayombo amewasihi madalali hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi mbalimbali akiwemo Diwani wa Kata hiyo, Ofisa Mtendaji Kata sambamba na Wenyeviti wa Mitaa kwani ushirikiano pekee ndio njia ya mafanikio katika Jamii yoyote.
MD Kayombo amesisitiza pia ulipaji wa ushuru kwa madalali hao kama ambavyo makubaliano baina yao na serikali yalivyo.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
0 comments:
Post a Comment