Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (mwenye fulana ya Bluu) na Mbunge wa Chalinze, Mhe.
Ridhiwani Kikwete wakifukia nguzo ya umeme kwa udongo ikiwa ni ishara ya
kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya
Tatu katika mkoa wa Pwani.
Watendaji kutoka kampuni ya Steg
International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo
pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu
ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza
ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI wa nishati na madini
,prof. Sospeter Muhongo,amezindua mradi wa umeme vijijini (REA)awamu ya
tatu katika mkoa wa Pwani na kudai mkoa huo utapewa kipaombele kwani ni
kimbilio la wawekezaji na ukanda wa viwanda.
Aidha amewataka watanzania kuacha kujidharau kupitia mradi huo kutokana ni mkombozi wa wananchi .
Mbali ya hayo,Pro.Muhongo anasema,mwaka
2007 kulikuwa na asilimia 2 pekee ya watumiaji wa nishati ya umeme
lakini kwa sasa kasi inakua ambapo imefikia asilimia 49.5.
Akizindua awamu ya tatu ya
mradi huo na kumtambulisha mkandarasi kutoka Tunisia kampuni ya Steg
katika mkoa huo,alisema ni wakati wa kuchangamkia fursa hiyo kwa kila
mtanzania mwenye mahitaji ya umeme.
Alisema katika awamu
hiyo,imetengwa kiasi cha sh.trilioni moja ambapo vijiji 3,559 vitafikiwa
nchini na mkoa wa Pwani vitafikiwa vijiji 150 vilivyokuwa havijafikiwa
kwenye awamu ya kwanza na ya pili.
“Malengo yetu ni kuvifikia
vijiji vyote 12,268 nchini ,kwa kutumia umeme kupitia Tanesco na mradi
huu wa umeme vijijini ili kila mmoja anufaike nao na kuondokana na
kutumia vibatari”alisema.
Hata hivyo ,Pro.Muhongo
alisema, wakati mradi wa REA awamu ya tatu ukianza katika maeneo
mbalimbali nchini ni lazima upelekwe katika taasisi ikiwemo
zahanati,shule na madhehebu ya dini .
Alisema mkoa wa Pwani ni mkoa kati ya mikoa iliyojikita katika viwanda na uwekezaji hivyo ni lazima nguvu kubwa ielekezwe huko.
Pro.Muhongo alimtaka mkuu wa
mkoa wa Pwani kuwaweka tayari wataalamu wake wa mkoa,na wataalamu wa
Tanesco ,REA,wabunge na meneja wa kanda ,ili kuweza kubainisha mahitaji
yote ambayo yatarahisisha kufanyiwa kazi na wizara.
Aliwaomba wananchi
watakaopitiwa na miundombinu ya umeme vijijini kutotaka fidia ili
serikali iweze kufanikisha malengo yake na kuinua maendeleo ya
watanzania.
Pro.Muhongo alisema kuwa fedha
zilizotengwa ambazo ni karibu trilioni moja zilizotengwa kwa ajili ya
mradi huo hazitakuwa sehemu ya fidia kwa ajili ya maeneo umeme huo
utakapopita.
“Bajeti iliyopangwa kutumika kwenye
awamu hii kwa nchi nzima ni mara tatu ya bajeti iliyopita huku fedha
hizo zikiwa ni za ndani hivyo wananchi wajitolee pasipo kudai fidia,”
alisema.
Waziri huyo,alieleza
kwamba,serikali imedhamiria kufikisha umeme kwa watanzania ,kwa malipo
yenye gharama nafuu ya.sh.27.000 sawa na majogoo mawili.
Pro.Muhongo,alimpongeza mkuu
wa mkoa wa Pwani,kwa kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji,pamoja na
mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete na wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa
kwa kupigania maendeleo ya majimbo yao.
Naye mkurugenzi wa REA Injinia,
Gisima Nyamo-Hanga alisema ,moja ya changamoto zinazowakabili ni baadhi
ya wananchi kudai fidia kwa maeneo ambayo miundombinu ya umeme
inapopitishwa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi
Evarist Ndikilo alisema kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya
wateja kuhitaji kuunganishiwa umeme lakini vifaa kama vile nguzo, mita
na nyaya ni vichache.
Ndikilo aliomba mkoa huo
uongezewe nguvu ya umeme megawatt 60 ambapo kwasasa wanapata megawati
38 hadi 40 ambazo hazikidhi mahitaji ukizingatia mkoa umesheheni
viwanda.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Chalinze Ridhiwani Kikwete alieleza mahitaji ya umeme ni makubwa katika
vijiji vilivyopo Chalinze .
Aliomba mahitaji mapya yaingizwe kwenye bajeti kwa lengo la kufanyiwa kazi katika bajeti ya 2017-2018.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini
Hamoud Jumaa alisema kuwa baadhi ya vijiji kama Gwata,Lukenge,Mpiji na
baadhi ya misikiti,shule na zahanati havina umeme hivyo kushindwa
kujiendeleza.
0 comments:
Post a Comment