Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwonya na kumwambia Mbunge wa Kawe, Halima
Mdee (Chadema), kwamba kadi za onyo kwa ajili yake zimeisha kutokana na
kushindwa kuhudhuria mahakamani siku ya kesi.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya
kubaini kwamba ilitolewa hati ya kumkamata mbunge huyo kwa kushindwa
kufika mahakamani.
Halima
Mdee alipotakiwa kujitetea aliinuka na kujieleza kuwa amefika
mahakamani hapo akiwa na nyaraka za safari ikiwamo tiketi na VISA na
kwamba taarifa za safari alimpa wakili.
Kwa
upande wa wakili wao, Hekima Mwesiga aliieleza mahakama kuwa nyaraka za
kuiarifu mahakama juu ya safari ya Halima Mdee nje ya nchi kwa bahati
mbaya hakuziwasilisha, alikuwa nazo Peter Kibatala ambaye alikuwa
akiendesha kesi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Tutaonana
wabaya katika hili ni lazima unapofanya kitu adabu yake ifuatwe, Wakili
hakufuata taratibu na Halima kabla ya kusafiri ulipaswa kutoa taarifa
mahakamani ili uweze kupata ruhusa ya mahakama lakini haukufanya hivyo.
“Sasa nafikiri wote tufuate taratibu za kuhudhuria mahakamani, Halima Mdee kadi zako za kukuonya zimeisha tafadhali,”alisema Hakimu.
Mdee
na wabunge wengine wa Chadema, Mwita Waitara, Saed Kubenea na makada
wao wanatuhumiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresa Mmbando.
Kabla
ya onyo hilo, mahakama ilisikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka
uliotolewa na Mrakibu wa Polisi, ambaye pia ni Msaidizi wa Operesheni
Ilala, Eugen Mwampondele.
Mwampondele alidai siku ya tukio alimwona Rafii Juma na Halima Mdee wakimkunja Theresa Mmbando ili awape nyaraka.
Shahidi
huyo alidai waliompiga Mmbando hawapo mahakamani. Washtakiwa katika
kesi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Diwani wa Kata ya
Kimanga, Manase Njema (56), Halima Mdee (37) na Mbunge wa Ukonga, Mwita
Waitara (40).
Wengine ni mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma (21)pamoja na Diwani wa Kata ya Saranga, Ephreim Kinyafu (33).
Inadiwa
kuwa Februari 27, 2016 katika Ukumbi wa Karimjee Wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam watu hao walimjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha
mwilini wakati wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment