Mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, unakabiliwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni mapoja na barabara zilizoharibika
Zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya taka kwenye
eneo moja kubwa la kumwaga taka nje ya mji mkuu wa Ethiopia Addis
Ababa.
Chanzo cha usalama kimesema kuwa watu
kadhaa hawajulikani waliko tangu maporomoko hayo yatokee siku ya
Jumamosi usiku. Mashahidi wanasema kuwa watu zaidi ya 150 walikuwa eneo
hilo, na inaminiwa kuwa wengi wao wamepoteza maisha.
Eneo hilo limekuwa likitumiwa kutupa
taka kutoka kote mjini Addis Ababa kwa zaidi ya miongo mitano.
Inaarifiwa kuwa mabanda mengi ya watu yamefukiwa chini ya taka na watu
wamekua wakitafuta vitu vyao. Serikali nayo imekuwa ikijenga kiwanda cha
kwanza barani Afrika, kwa lengo ya kuibadili taka hiyo kuwa nishati
karibu na eneo hilo.
Sserikali ina mpango wa kuchoma taka na
kuugeuza kuwa umeme. Hata hivyo wa eneo hilo wamekuwa wakisaka eneo hilo
kujitafutia riziki.RFI
0 comments:
Post a Comment