Ilikuwa mwaka 1938 wakati kijana mdogo
wa miaka 29 aliejulikana kama Nicholas Winton ambae aliekuwa ni dalali
wa hisa (stockbroker) jijini London aliamua kuacha shughuli zake na
kwenda nchini Czechoslovakia. Lengo la safari yake ilikuwa ni kuwaokoa
watoto wa Kiyahudi 669 waliokuwa katika kambi ya wakimbizi.
Nicholaus alitengeneza mpango wa
kuwavusha kutoka Czechsolovakia na kuwapeleka watoto hao England;
alipofika England alifanya kazi ya kutafuta familia za Waingereza na
kuzishawishi ziwachukue watoto hao kwa lengo la kuwalea.
Katika mpango huo kabambe, Nicholaus
alichukua magari 8 na kwa umakini na usiri mkubwa alifanikisha zoezi
hilo la kuwaokoa watoto hao. Nicholaus alifanya siri ambayo hata mkewe
hakuweza kujua. Miaka 50 baadae, mkewe wakati anapekua pekua vitu,
aliweza kuona kitabu kikiwa kimefichwa kwenye dari. Kitabu hicho cha
similizi kinachojulikana kama (scrapbook) kilikuwa na majina na picha za
watoto wote waliokolewa na Nicholas kwa takribani miongo 5 iliyopita.
Mkewe, Greta aliamua kuichukua simulizi hiyo na kumpelekea Elisabeth
Maxwell ambae alikuwa mtafiti wa mauji ya kimbari ya Wayahudi
(Holocaust) na barua za hao watu waliokuwa watoto nyakati hizo. Kulikuwa
na mwitikio kutoka kwa watu zaidi ya 200 kati ya wale 669 katika ile
orodha ya watoto kwa miongo 5 iliyopita kwa wakati huo.
Dunia iliyobakia nikiwemo mimi nawe
msomaji wangu ilikuja kuifahamu simulizi hii kupitia filamu-simulizi
(documentary) iliyotengenezwa na kituo cha habari cha BBC yenye jina
That’s life (yaani haya ndiyo maisha). Nicholaus alialikwa kama mmoja wa
wahudhuriaji wa katika onesho hilo. Kile kitabu chake cha kumbukumbu
kikafunuliwa na maelezo kutolewa, na aliekuwa mwenyeji wa hafla hiyo
akauliza umma uliokuwa umehudhuria ambao walikuwa wameokolewa kutoka na
uamuzi wa Nicholas kuokoa maisha yao. Zaidi ya watu 20 walisimama wakiwa
wamemzunguka Nicholas na kupigia makofi ya kumpongeza na kumshangilia
Nicholas.
Waweza kuiona video hiii kupitia tovuti ya www.youtube.com/watch?v=6_nFuJAF5F0
na kumwona mtu mkuu alieamua kugusa maisha ya watu na vizazi vingine
baadae maishani. Kwa uchache kati ya watu aliowaokoa ambao ni maarufu
katika jamii ni pamoja na Alf Dubs, Baron Dubs (iliezaliwa mwaka 1932)
na alikuwa Mbunge wa bunge la Ungereza kwa kupitia chama cha Labour.
Heini Halberstam (aliezaliwa mwaka 1926) na alikuwa bingwa wa hisabati.
Renata Laxova (aliezaliwa 1931), alikuwa daktari bingwa wa masuala ya
vinasaba vya watoto (peadiatric geneticist). Wengine ni Joe Schlesinger
(aliezaliwa 1928) alikuwa mtangazaji wa vipindi vya televisheni huko
Canada na muandishi wa vitabu. Na wa mwisho kumtaja katika makala hii
katika orodha ndefu ni Yitzchok Tuvia Weiss (aliezaliwa 1926), alikuwa
Rabi Mkuu Jerusalem. Rabi ni mwalimu wa dini ya kiyahudi.
Mpaka mwaka 2015 shirika la habari
Uingereza BBC liliweza kuwasiliana na zaidi ya watu 200 kati ya
waliokuwa watoto 669 walioweza kuoka na zahma la mauji ya kimbari.
Kutokana na maamuzi aliyoyafanya
Nicholas, amefanikuwa kukusanya tuzo za heshima chungu nzima ikiwemo
kupewa cheo cha heshima na ushujaa kutoka kwa malkia Elizabeth II wa na
kuwa SIR NICHOLAS WENTON. Jamhuri ya Czech ilimpa Sir Nicholas Wenton
tuzo ya heshima ya Simba Shujaa; Kwa upende wake Rais wa awamu ya 7 nchi
Israel Ezer Weizman aliwahi kumpa tuzo ya heshima kwa niaba ya Taifa
lake.
Nimeguswa sana na watu wengie pia wameguswa na maamuzi ya Nicholas aliemua kuhatarisha maisha yake na kutumia gharama zake kwenda katika kambi kwa lengo la kuokoa watoto ili mkono wa mauaji ya kimbari wa Adolf Hitler usiwafikie. Miaka 50 baadae simulizi hiyo iliwekwa wazi na watu wengi kujua juhudi na “innitiatives” za Sir Wenton alizofanya akiwa kijana mdogo.
Napiga picha ya initiative ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paulo Makonda ya kunzisha vita dhidi ya
uuzwaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam. Kimsingi watu wengi
wamepokea taarifa hii kwa mshangao kuna kwamba “atafika wapi!”
Aidha kuna wengine wanamkejeli kama mtu
anaejaribu kufunika aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kufeli hususan
mkoani Dar es Salaam. Wengina wakidhani anatafuta umaarufu. Kila mmoja
kwa hisia zake.
Binafsi nampongeza Paulo Makonda kwa
nafasi yake na uzalendo wake kwa nchi uamuzi wa kuchukua hatua ya
kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vilivyo chini ya ofisi yake
na kutoa amri ya watuhumiwa wanaohusika kukamatwa ili wahojiwe na
wengine kusimamishwa kazi ili uchunguzi uendelee pasipo wao kuathiri
uchunguzi kama watakuwa kazini.
Nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni
njema. Amenuia kupiga vita vizuri dhidi ya biashara ambayo inaua hatima
ya vijana wa Kitanzania. Tukumbuke matokeo ya vijana kutumia “unga” ni
kuwaharibia kesho yao na mchango wao ambao wangeweza kuutoa katika
ujenzi wa taifa hili.
Ilitakiwa Watanzania kwa nafasi zozote
tulizonazo tusimame na Paulo Makonda kwa kuwa anachokipinga ni kitu
kibaya. Michelle Obama wakati mmoja aliwahi kusema kuwa “kumpiga vita
mmoja wetu ni kutupiga vita sote” Kwa mantiki hiyo kumpiga Paulo Makonda
nia yake njema ni kupinga sheria za nchi zenye lengo la kuzuia
matumizi, uuzwaji na usambazaji wa madawa ya kulevya.
Ni ukweli ulio wazi kuwa, mtu yeyote
mwenye mguso maishani alijengewa mazingira mazuri ya kumsaidia kufika
ndoto zake maishani. Mihidarati ni kitu ambacho kinaweza kuharibu tabia
njema na mwenendo wa vijana na watoto kuifikia kesho yao. Hivyo basi
tunawajibika kuipingwa kwa ngivu zote.
Yawezekana si kila mtu ana nafasi ya
kuwa kwenye vyombo vya dola ili kutumia misuli kuzuia utumiaji wa
mihadarati au usambazaji; kutokuwa na nafasi kama ya Paulo Makonda au
IGP Ernest Mangu, bado tuna jukumu la kupigana kwa kupitia kuwatia moyo
wapiganaji walio-mstari wa mbele kwa njia ya kuwaombea kwa Mungu au hata
kupaza sauti kupitia vyombo vya habari. Na tukiachukulia mfano wa
wapenzi wa soka anafahamu nguvu ya kumshangilia mchezaji au wachezaji
wanapofanya vizuri.
Nicholas alifanya maamuzi ya kuokoa
watoto 669, miaka 50 baadae, watu wale walikuwa watu wenye mguso akiwemo
muandishi wa habari, daktrari bingwa wa watoto, mwalimu mkuu wa dini na
wengine wengi. Juhudi za Makonda zikifanikiwa Dar es Salaam na kila
mmoja akacheza nafasi yake kutimiza wajibu wake kukaba ili wasambazaji
wasiendelee kuuzaa katikati yetu, ni watu wangapi tutawaokoa?
Kama Mtanzania mzalendo, sioni kama
mihadarati ina nafasi ya kuongeza thamani katika maisha ya watoto na
vijana kama wahanga wakubwa wa mihadarati.
Rai yangu ni kuwa sisi kama wanajamii
tunawajibika kwa pamoja kuijenga nchi hii. Jirani akiharibikiwa au mtoto
wa jirani akiharibikiwa madhara yake yana uwezekano kwa upande mmoja au
mwingine kugusa maisha yangu au watoto wangu. Njia rahisi ni kuamua
kupigana kuzuia madhara yasisambae kuliko kuachilia yasambae.
Rais John Magufuli kampongeza IGP Mangu
kwa kuchukua hatua ya haraka za kinidhamu kwa watuhumiwa ndani ya Jeshi
la Polisi ili kupisha uchunguzi ufanyike.
Tukipanda mbegu njema kwa kugusa maisha
ya wengine, ipo siku tutavuna taji ya heshima kwa mrejesho wa watoto
wetu na vijana wetu kuwa na mguso chanya kwenye jamii. Ili jamii yetu
iwe na uzalishiaji wenye tija (effective production) mihadarati lazima
ipigwe vita ndani ya mipaka yetu. Paulo Makonda kaonesha mfano, kwa
pamoja tumuunge mkono.
fmatuja@hotmail.com
0 comments:
Post a Comment