Tanzania
imeingia rasmi kwenye mfumo maalum wa kimataifa wa kupata huduma za
afya ya UKIMWI kwa njia ya simu bila malipo mfumo ambao umefadhiliwa na
nchi ya Marekani.
Akizindua
mfumo huo Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser amesema
mfumo huo utawafikia zaidi ya watu laki nane huku lengo kuu la mfumo huo
likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi
kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 0.0.
Amesema
watu wote ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi
hadi kufikia mwaka 2020 wawe tayari wamepimwa kwa asilimia 90, asilimia
90 waanze kutumia dawa, na asilimia 90 kiwango chao cha maambukizi kiwe
kimepungua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TAYOA nchini Bw . Peter Masika
amesema katika ufadhili wa mfumo huo wao wakiwa ni wasimamizi wa mfumo
watahakikisha unawafikia watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma
muhimu za kiafya na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia
mfumo huo ili kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment