Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo jana mkoani
Mbeya (hawapo pichani) ikiwa ni moja ya malengo ya ziara yake ya kikazi
mkoani humo. Kulia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni Afisa
Michezo Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama
vya michezo jana mkoani Mbeya . Picha na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya.
Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
Wadau wa
michezo mkoni Mbeya wametakiwa kuendeleza mshikamano walionao ili
kuifanya sekta ya michezo kuwa chanzo cha kuongeza fursa za ajira kwa
vijana pamoja na wataalamu wengine wa michezo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel amesema hayo leo jijini Mbeya alipokuwa akiongea na baadhi ya
viongozi wa vyama vya michezo mkoani humo ikiwa ni moja ya malengo ya
ziara yake ya kikazi mkoani humo.
“Nimefurahishwa
na mkoa wa Mbeya kuwa na mipango ambayo imewafanya vyama vya michezo
kuendeshwa bila kuwa na migogoro, hii ni hatua nzuri imenipa moyo,
mkishikamana vizuri mtafanikiwa sana katika malengo yenu ya michezo”
alisema Prof. Ole Gabriel.
Ili
kuhakikisha michezo inakuwa na tija kwa mkoa wa Mbeya na taifa, Prof Ole
Gbriel ametaka viongozi hao kuwa na mkakati wa kimkoa wa kubadilisha
fikra za watu katika michezo na kutambua kuwa zipo fursa nyingi katika
michezo yote bila kubagua aina ya mchezo.
Awali
akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya michzo, Prof. Ole Gabriel
ameataka wadau hao kutambua kuwa michezo inaanzia katika ngazi ya chini,
hivyo ni wajibu wao kuendeleza michezo kwa kubadili fikra za wazazi,
vijana, walezi kuipenda michezo kwa kuwa inamchango mkubwa katika ajira,
pato la familia pamoja na uchumi wa taifa.
Akimkaribisha
Katibu Mkuu Prof. Ole Gabriel, Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni
Afisa Michezo Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba amesema kuwa Serikali ya
mkoa inaendelea kushirikiana na wadau wa michezo yote kwa kuzingatia
michezo ni ajira, udugu katika kujenga umoja wa michezo kimkoa na taifa.
Akizunguzia
mpira wa miguu, Katibu Msaidizi Chama cha Mpira wa Miguu Mbeya (MREFA)
Lucas Kubaja amesema kuwa mpira wa miguu unachezwa kuanzia ngazi ya
chini, wilaya zote hadi mkoa.
Kubaja
ameongeza kuwa mkoa unapokuwa na timu nyingi za michezo mbalimbali
katika ligi za michezo hiyo inasaidia kuongeza fursa za kiuchumi kwa
wakazi wa mkoa wa mbeya kunapokuwa na timu zinazokuja kucheza mechi zao
kwenye ligi husika.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wadau hao wa michezo wamemweleza Katibu Mkuu mwenye
dhamana ya michezo kuwa michezo mingi mkoani Mbeya inakabiliwa na
changamoto ya kutokuwa na viwanja vya michezo hatua ambayo inarudisha
nyuma ukuaji wa michezo mbalimbali.
Vyama nya
michezo vilivyoshiriki mkutano huo huo ni mpira wa miguu (MREFA), mpira
wa pete (CHANETA), mpira wa kikapu, chama cha makocha, riadha, vishale
pamoja na pool table.
0 comments:
Post a Comment