Mfalme wa Morocco, Mohamed VI
Wizara ya
Mambo ya Nje ya Morocoo inamtuhumu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa
Afrika (AU) kuwa pingamizi kwa nchi ya Morocco kurejea katika Umoja wa
Afrika.
Katika
taarifa iliyotolewa Jumatano hii, Morocco inamtuhumu Nkosazana
Dlamini-Zuma, raia wa Afrika Kusini, "kujaribu kwa kutumia ujanja mpya
wa kuzuia uamuzi wa Morocco wa kurejea kwenye nafasi yake ya asili na
halali katika familia yake ya kitaasisi ya Afrika."
Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa miezi kadhaa amekua amekua akifanya jitihada za kuirejesha nchi yake katika Umoja wa Afrika.
Morocco
ilijiondoa kutoka Umoja wa Afrika tangu mwaka 1984 kwa kupinga dhidi ya
kukubaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharaw (Sadr), ambayo
inaicukuliakama sehemu ya ardhi yake.
Katika
taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imemtuhumu Bi
Dlamini-Zuma kwa "kuchelewesha bila sababu ya kueleweka, ombi la Morocco
kwa wanachama wa Umoja wa Afrika."
Morocco
inasema kuwa ilimtuma ombi lake la kutaka kurejea katika Umoja wa Afrika
tangu mwezi Septemba 2016 na inasema kuwa Nkosazana
Dlamini-Zuma "anaendelea na kasi yake kuzuia" faili ya Morocco, "kwa
kuishitukiza utaratibu mpya, usiyokuwa wa kawaida na msingi msingi
wowote".
Mwenyekiti
wa Tume ya Umoja wa Afrika amefutilia mbali barua ya nchi wanachama wa
Umoja wa Afrika zinazoiunga mkono, kwa mujibu wa serikali ya Morocco.
Kurudi kwa Morocco katika Umoja wa Afrika lazima kupitishwe kwa kura ya nchi wanachama kwa wingi wa theluthi mbili ya kura.RFI
0 comments:
Post a Comment