Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iramba
Magharibi Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30,
2019.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amesema Serikali inawahitaji madaktari na wauguzi ili waende kutoa huduma
katika hospitali, vituo vya afya na zahanati.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 30, 2019)
alipozungumza na wanafunzi wa mwaka wa tano wanaosomea udaktari Chuo Kikuu
cha Dodoma.
Waziri Mkuu amewataka wanachuo hao wasome kwa bidii
ili waweze kufaulu masomo yao na kuapata sifa zitakazowawezesha kuajiriwa au
kujiajiri.
Waziri Mkuu amekutana na wanafunzi hao
katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, alipokwenda kumjulia hali Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga.
Akiwa hospitalini hapo, pia Waziri Mkuu alimjulia
hali Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Makunda ambaye anamuuguza mtoto wake,
Tunu Kikula.
Wengine aliowajulia hali ni pamoja na Mbunge wa
Viti Maalum, Sabrina Sungura ambaye amelazwa hospitalini hapo pamoja na
wagonjwa wengine.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu amewapongeza madaktari hao ambao ni wanafunzi.
Amesema madaktari hao wamekuwa wakitoa msaada
mkubwa kwa madaktari bingwa katika kuwahuduma wagonjwa wanaofika
hospitalini hapo.
0 comments:
Post a Comment