Umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Serengeti (uvccm),
wakiongozwa na katibu wa uvccm wilaya Serengeti ndg, Alphonce Patrick Muyinga
(Black) Pamoja na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ( W ) Ndg, Muhochi Leo Pamoja na vijana wilaya ya Serengeti
kata ya Mbalimbali kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo Mh.John Ng'oina
wameazimisha sherehe za kuzaliwa ccm kwa kukagua miradi katika kata hiyo ya
Mbalimbali.
Pamoja na kusikiliza kero za wana nchi katika kata hiyo. pia
diwani wa kata hiyo kwa niaba ya wana nchi alieleza kero ya maji katika kijiji
hicho Ambacho Kuna mradi uliopaswa kukamilika mwaka Jana mwenzi wa 6 lakini
mpaka Sasa unasuasua na kero ya maji imezidi
Kua kubwa hasa kwa vijiji vya kata hiyo.
Pia Mh.Diwani huyo
ameeleza juu ya kata yake yenye vijiji vitano Kua na kituo cha afya kimoja, mpka Sasa ametafuta wahisani wa
kusaidia huduma hiyo. wamejitokeza lakini changamoto ni nyingi katika wizara ya
afya wanazokutana nazo.
Pia, Umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Serengeti waliongea na
vijana kuhusu elimu ya mikopo inayotolewa na serikali kwa vijana. Na kuwa
kumbusha vijana wa kiume kuwaepusha mabinti na swala la tohara. Kwa maana ni unyanyasaji kwa watoto
wa kike.
Pia, Mabinti wawe jasiri kwa kutoa taarifa kwenye vyombo
vya ulinzi na usalama pale wanapo
lazimishwa kufanya tohara.
Vilevile,Umoja wa
vijana ccm wilaya ya Serengeti uliwakumbusha vijana kuwa, jukumu la kulinda
amani ya nchi yetu ni la kila mtanzania.
Na Kuwaonya Kua vijana tusikubali kutumika kwa maslahi ya mtu
binafsi. Pia tuwe mstali wa mbele kusema mazuri yanayo tendwa na serikali yetu.
Lakini tusiwafumbie macho viongozi Bila kujali ni viongozi wa kisiasa au
serikali Hata Kama wanatokana na ccm, Kama dhamira yao sio nzuri kwa masilahi ya
taifa na ccm
0 comments:
Post a Comment